WALIYO TAFUNA FEDHA ZA TASAF KUKABILIWA NA MASHITAKA YA UHUJUMU UCHUMI.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Watu wanne wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha akiwimo Mtumishi mmoja wa serikali wakikabiliwa na mashitaka mawili tofauti ya utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 90 fedha za miradi ya TASAF.
Akiongea na Motive Media Tanzania ( MTV) Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha Zainabu Ngailo, Ameeleza kuwa watu hao wanakabiliwa na kesi hizo baada ya uchunguzi wakina waliyoufanya baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alipo wasimamisha kazi baadhi ya watumishi hao na kuwataka Takukuru kuchunguza tuhuma hizo.
Ngailo ameeleza kuwa baada ya uchunguzi huo uliweza kuwabaini watu wanne ambapo amewataja kwa majina yao ni Amani Elifatio Mlay (40) ambaye alikuwa mratibu wa TASAF Arusha Jiji, Godgive Misque Sangka (41) ambambaye ni M.kiti wa Mtaa wa Moivo, Cecilia Domick Zumba (37) Mfanyabiashara Jijini Arusha na Gerson Sanare Mollel (60) fundi ujenzi.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi mbili tofauti katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambopo shitaka la kwanza ni kesi namba 11965 ya mwaka 2024 ambapo washitakiwa ni Amani Elifatio Mlay, Godgive Misque Sangka, Cecilia Domick Zumba, ambapo wanakabiliwa na kesi ya ubadhilifu wa fedha kiasi cha shilingi Milioni 26.262, ( 26,262,040 Milioni ) katika ujenzi wa jengo la utawala katika Shule ya Msingi Moivo.
Ambapo washitakiwa hao wamehusika kufanya malipo kinyume na utaratibu wa mkataba wa zabuni kwa kuto walipa wazabuni waliyofanya kazi pamoja na usambazaji vifaa vya kazi ya ujenzi na hawajalipwa fedha zao na badala yake akalipwa mzabuni ambaye hajafanya kazi hiyo huku mradi huo ukiendelea kusuasua na bado hadi sasa haujakamilika.
Aidha katika shitaka la pili lenye kesi namba 11512 ya mwaka 2024 ambapo washtakiwa ni watatu ambao ni Amani Elifatio Mlay, Cecilia Domick Zumba na Gerson Sanare Mollel, wanao wanakabiliwa na ubadhilifu wa fedha shilingi milioni 62.916, ( 62,916,000 ) za ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi Ngarenaro.
Ambapo pia kuna wazabuni waliyo Sambaza vifaa kazi na hajalipwa na badala yake akalipwa mzabuni mwingine kinyume na utaratibu wa makubaliano ya uzabuni na aliyo lipwa fedha hizo siyonaliye fanya kazi hiyo ya ku-supply vifaa hivyo vya ujenzi.
Aidha Ngailo ameeleza kuwa kesi ya kwanza yenye namba 11965 ya mwaka 2024 washtakiwa wote wametenda makosa hayo kinyume cha vifungu vya sheria ya makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujinufaisha wao wenyewe pamoja na uhujumu uchumi kama inavyo elezwa katika kifungu cha sheria ya Takukuru kifungu namba 22, 30 na 31, na kifungu sheria namba 265 cha makosa ya jinai.
Huku katika mashitaka ya pili yanayo wakabili washitakiwa watutu, wanashitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi katika kifungu cha 10(1), 57(1) na 60(2) cha mwenendo wa sheria ya uhujumu uchumi
Aidha Kamanda Ngailo ametoa rai kwa wananchi kutoendelea kutoa wala kupokea rushwa kwa jambo lolote lile wala kujihusisha na viashiria vyoyote vya rushwa kitu ambacho ameeleza wao kama Taasisi ya kupambana na rushwa hawata vumilia vitendo hivyo vinavyo pelekea upotevu wa haki kwa baadhi ya watanzania.
Comments
Post a Comment