DC KUBECHA NA DED HAMSINI KUIFANYA TANGA KUWA LANGO LA KIBIASHARA AFRIKA MASHARIKI.

ENG. HAMSINI ATAKA UJENZI WA KISASA MASHULENI PAMOJA NA MIUNDOMBINU YAKE.

By Lucas Myovela - Tanga.

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha, Amewataka watumishi kuwa na umoja kattika utendaji kazi ili kuifanya Tanga kuwa kitovu cha kibiashara katika ukanda wa nchi za Afrika ya Mashariki na kiwa Jiji la Kisasa lenye kuvutia wakati wote, Huku Mkurugenzi wa Jiji hilo Eng. Juma Hamsini akihaidi kuifanya Tanga kuwa Smart City na kuboresha mindombinu mashuleni.

Kubecha ameyasema hayo wakati aliposhiriki kikao cha Baraza la Madiwani Jiji la Tanga Agosti 28,2024 kikao cha uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji hilo.


"Nawaombeni sana Tushirikiane na Tushikamane kwa Kuchapa kazi ndani ya Halmashauri ya Tanga , imani yangu Tanga Inaenda Kuwa Jiji la Kisasa lenye Kuvutia Wawekezaji na Watu Mbalimbali Kulitembelea Lakini pia Kuhakikisha ahadi zote za Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alizohaidi zitatekelezeka kwa wakati ili Kulinda imani yake ya Kazi Iendelee". Amesema Kubecha.

Akiongea katika kikao hicho, Eng. Hamsini amewataka wasimamizi wa miradi ya elimu na maendeleo katika Jiji la Tanga kutotumia madawati ya mbao katika shule za kata ili kuleta hadhi inayostahili kwa shule hizo.


"Nimekuja tushirikiane katika maendeleo na tuijenhe Tanga iwe na hadhi ya Jiji kweli kweli niwaombe maafisa elimu kuanzia sasa tusipeleke madawti ya mbao katika shule zetu za kata tupeleke madawati ya kisasa ili wanafunzi wanapo soma wasiwe na msongamano maana Rais wetu tayari ameweka miundo mbinu sahihi ya elimu hapa nchini". Amesema Hamsini.


"Pia katika ujenzi wa madarasa tunapo yajenga yawe yenye hadhi na miundombinu yote ya kisasa. Milngo yangu ipo wazi kwa yeyote mwenye mawazo ya kimaendeleo katika kila idara aje tushauliane lengo langu ni sote tuungane kuijenga tanga yetu kuwa mji wa kisasa wa kibiashara". Ameongeza Hamsini.

Kikao hicho cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga ni kikao cha kufunga hesabu za mwaka 2023/2024, pamoja na uchaguzi wa Naibu Meya na wenyeviti wa kamati za kudumu za Halmashauri na kimengozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloow.


Aidha kikao hicho kimempitisha Mhe. Rehema Mhina, kuwa Naibu Meya kwa kipindi cha pili, na kulidhia kuwarudisha kwenye nafasi zao Wenyeviti wa Kamati za kudumu. 

Pia ikilumbukwe hiki ni kikao cha kwanza cha Baraza hilo kufanyika tangu kuhamia Jiji la Tanga kwa Mkurugenzi Eng. Juma Hamsini, na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Japhari Kubecha kutokana na mabadiliko aliyo yafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Aidha hicho kimeudhuliwa na Mkuu wa Wilaya Aliongozana na Katibu Tawala wa Wilaya Dalmia Mikaya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tanga pamoja na wakuu wa idara mbalimbali wa Jiji la Tanga.





Comments