MAVUNDE AWASHUKIA VIKALI WANAOTAKA KUVURUGA AMANI YA MIRERANI KWA KUANZISHA CHOKOCHOKO JUU YA SOKO LA MADINI YA TANZANITE.

ADAI HAKUNA WAZIRI YEYOTE ALIYO JUU YA SHERIA ZA MADINI  NA KUTENGUA MAAGIZO YA RAIS.

Na Lucas Myovela , Mirerani.


Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema kuwa soko la Madini ya Tanzanite limekuwa likishuka kila Siku katika soko la Dunia hivyo Wizara yake imekuja na mpango kazi wa kuhakikisha soko la Madini hayo linapanda ili wafanyabiashara wa Tanzanite waweze kunufaika na Madini hayo.

Mavunde alisema hayo wakati akiwahutubia wafanyabiashara wadogo Kwa wakubwa wa Tanzanite,wamiliki wa migodi ya Tanzanite,wachimbaji na wauzaji katika Mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya ukuta wa Madini ya Tanzanite katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Alisema baada ya kuona soko la Madini ya Vito(Tanzanite) lenye ushindani mkubwa katika soko la Dunia Wizara yake iliunda Kamati maalumu iliyoshirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Madini ili wafanye utafiti wa ndani ya nchi na nje na kuja na majibu sahihi ya kuboresha Biashara ya Tanzanite ili iweze kunufaisha Wananchi na Serikali kuingiza mapato.


Waziri Mavunde alisema miongoni mwa mapendekezo ya Kamati ni kubadilisha Sheria ya madini ya Tanzanite na kanuni zenye lengo la kuboresha Biashara hiyo Kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo na hilo kimefanikiwa na kila Mdau wa Tanzanite alishirikishwa katika kutoa maoni.


"Hakuna Waziri yoyote Duniani katika Serikali yoyote ya nchi yoyote anayeweza kutengua maagizo ya Rais au Waziri Mkuu na kusema kuwa soko la Madini ya Tanzanite litabaki kuwa katika Mji wa Mirerani na Madini ya Tanzanite yataongezewa thamani ndani ya ukuta wa Mirerani kama viongozi Wakuu wa nchi walivyoagiza na sio vinginevyo".Ameeleza Waziri Mavunde.

"Jengo la Tanzanite City linalogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambalo limefikia asilimia 80 za kukamilika kwake na Mkandarasi anakabidhiwa pesa yake nyingine ya kumaliza kazi hiyo hadi kufikia 99% ya  kazi wiki ijayo atapokea fedha hizo ili amalize ujenzi wa jengo hilo na hapo ndio patakuwa nyumbani Kwa madini ya Tanzanite na Wale wenye kuwaza soko hilo kuhama waache kuwaza hilo na wasahau". Amesema Mavunde.


"Jengo la Tanzanite City Ni jengo la kimataifa hivyo eneo hilo linapaswa kuwa la kimataifa na Halmashauri inapaswa kuwajibika Kwa hilo ikiwa ni pamoja na kupanda miti eneo husika ili kuwa na maadharani mazuri ya kuvutia" alisisitiza Mavunde.

Naye Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alimshukuru Waziri Mavunde Kwa kumaliza utata wa soko la Madini ya Tanzanite kuendelea kuwa katika Mji wa Mirerani kwani baadhi ya watu na wanasiasa walikuwa wakiwayumbisha wafanyabiashara wa Tanzanite kuwa soko hilo litahamia katika Jiji la Arusha.


Sendeka alisema na kuwasisistiza wafanyabiashara wa Tanzanite Mirerani kuhakikisha wanaongeza thamani madini hayo ili waweze kunufaika nayo Kwa kufanya Biashara ndani ya ukuta ikiwa ni pamoja Na kulipa kodi zote za Serikali bila kukwepa.


"Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa walishasema soko la Madini ya Tanzanite Kwa Sasa lifanyike ndani ya ukuta wa Mirerani Na jengo la Tanzanite City likikamilika Biashara zote zihamie hapo na hayo ndio maagizo na hakuna Waziri au kiongozi yoyote anaweza kutengua Kwa Sasa na wanaopitapita kulaghai watu eti soko hilo litahamia sehemu nyingine ni kujidanganya". Alisema Sendeka.


Kufuatia kauli hiyo ya Waziri Mavunde wafanyabiashara wa Tanzanite wameonesha kufurahishwa na msamao huo wa serikali na kusema kuwa Kwa Sasa mji wa Mirerani na vitongoji vyake utainuka kichumi ikiwa ni pamoja na Wananchi kunufaika na rasilimali hiyo baada ya chokochoko nyingi zinazo enezwa na watu waaiyo penda maendeleo ya nchi hasa katika madini hayo adhimu ya Tanzanite.




Comments