MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI YAFUNGULIWA YAANZA KWA KIWANGO CHA JUU.
Wakulima,Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Kaskazini wametakiwa kuyatumia vyema maonyesho ya Kilimo ya Nanenane katika viwanja wa Themi Mkoani Arusha ili kuweza kujiinua kiuchumi kwani maonyesho hayo yana fursa kubwa kwao.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu wakati akifungua maonyesho hayo ya 30 katika viwanja hivyo baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho na kujionea zana za kilimo,mbegu Bora na za kisasa,Madume ya ng'ombe wa kisasa na ufugaji Bora na wa kisasa wa Samaki.
Alisema serikali imejenga mazingira mazuri ya kuboresha sekta ya kilimo.mifugo Na uvuvi hivyo Basi wahusika katika sekta hiyo wanapswa kuiunga mkono Serikali kwa kujitoa ili waweze kuinua uchumi wa mtu mmoja ama ushirika.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro alisema maonyesho ya Nanenane ni nguzo kuu ya uchumi Kwa Kanda ya Kaskazini hivyo wakulima,Wafugaji na Wavuvi Kanda hiyo wanapswa kuchangamkia fura hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi kwani sekta hiyo Serikali imewekeza mamilioni ya fedha Kwa ajili yao.
Alisema asilimia 90 ya watanzania wanategemea sekta hiyo na ndio maana Serikali imewekeza mamilioni ya fedha na itasikitisha kuona Wananchi wanakaa kimya bila kuchangamkia mamilioni hayo Kwa ajili ya kujiendeleza Kwa lengo la kujikomboa kiuchumi.
Babu amewahimiza wawekezaji kuuza zana za kilimo kwa bei rafiki ili zana hizo ziweze kuwasaidia wakulima katika kujikomboa kiuchumi kwani Bei alizoona katika mabanda ziko juu na haamini kama zinaweza kununuliwa na wakulima wadogo wadogo wadogo ambao Ni wengi katika Kanda hii Na nchi kwa ujumla.
Alisema wakulima wadogo ni wengi hapa nchi Na ndio nguzo ya nchi hivyo nao wanapaswa kusaidiwa ikiwa ni pamoja na kuuziwa zana za kilimo Kwa Bei Rafiki ili watumie katika Kilimo kuliko hivi Sasa wanatumia jembe la mkono.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwahimiza wakulima kulima kisasa ikiwa ni pamoja na kutumia mbegu za kisasa zenye kuhimili nyakati zote za majira ya mvua na kiangazi ili ziweze kuota Kwa wakati muafa Kwa kutumia mbolea ama kutotumia mbolea.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maonyesho ya Nanenane Mkoani Arusha ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha (RAS),Missaile Mussa alisema kuwa maonyesho hayo mwaka huu yameshirikisha viongozi wote wa Serikali na vyama vya ushirika katika Kanda ya Kaskazini Na maandalizi yalianza aprill 24 mwaka huu.
Mussa alisema wakuu wa Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara,Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na wenyeviti wa Halmashauri wote walishirikishwa katika kuhimiza wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda hiyo kushiriki maonyesho hayo lengo likiwa kuwainua kiuchumi.
Comments
Post a Comment