DHAMANA YA BONI YAI BADO NI KIZUNGU MKUTI.

KWA MARA YA KWANZA MAWAKILI WA SERIKLI KUMTETEA MTUMIWA KIUSALAMA.

SIRI KUBWA NDOA NYINGI KUVUNJIKA.

===============

KWA UFUPI KESI YA BONI YAI.

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu tarehe 19 Septemba 2024, akikabiliwa na mashtaka mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na sheria za makosa ya mtandao.


Kosa la kwanza linalomkabili Boniface Jacob linahusu kuchapisha taarifa za uongo mnamo tarehe 12 Septemba 2024, ambapo alidai kuwa Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kwa kupotea kwa wanafamilia wa hizo familia.


Kosa la pili, ambalo lilitokea tarehe 14 Septemba 2024, linahusiana na kuchapisha taarifa nyingine za uongo zinazosomeka ‘Polisi wanatesa watu na kuua ndio kazi wanaweza’. Boniface amekana mashtaka yote hayo.


Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Nasoro Katuga, pamoja na wenzake watano, umeiomba Mahakama ya Kisutu kumtaka mtuhumiwa Boniface Jacob kuruhusu wapelelezi kuingia kwenye simu zake za mkononi na akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) ili kukamilisha upelelezi unaohusiana na makosa hayo ya kimtandao.


Aidha, Wakili wa Serikali aliiomba Mahakama izuie dhamana ya mtuhumiwa kwa ajili ya usalama wake. Ombi hili lilitolewa na mwendesha mashtaka kwa hoja kuwa kuna hatari za kiusalama endapo mtuhumiwa ataachiliwa kwa dhamana.

VICHA VYA HABARI MAGAZETINI LEO IJUMAA SEPTEMBA 20, 2024.













Comments