ENG. HAMSINI AWATAKA WATUMISHI KUHAKIKISHA MIRADI YA SERIKALI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA UNAOTAKIWA ILI JAMII INUFAIKE NA HUDUMA ZA SERIKALI.
WATUMISHI WAMSHUKURU ENG. HAMSINI KWA KUWAKUTANISHA PAMOJA KWA MAENDELEO YA JIJI LA TANGA.


Kikao hicho kilikuwa na lengo la kukumbushama uwajibikazi kazini na kufanya kazi kwa weredi kwa mujibu wa viapo vya kazi kwa kila mtumishi,kufahamiana, kuweka mikakati ya pamoja, na kutatua changamoto za kiutendaji katika Jiji hilo.

"Ndg. Viongozi wenzangu niwaombe sana hasa wakuu wa idara na kila mmoja kwa nafasi yake ya utumishi kuhakikisha miradi hii tuliyopewa inakamilika kwa wakati, na kwa kuzingatia ubora, ili jamii inufaike na mipango ya Serikali ya kuwasogezea huduma karibu". Amesisitiza Hamsini.

Aidha katika hatua nyingine watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wamempongeza Mhandisi Hamsini kwa kuwaleta pamoja na kukumbushana majukumu ya kiutendaji na kuahidi wataenda kutenda kazi kwa weledi na bidii kwa maslahi mapana ya serikali.
Pia watumishi hao wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini Eng. Hamsini na kumpa jiji la Tanga na kueleza kuwa kwasasa wanaiona Tanga Mpya ambayo ilikuwa ndito ya kila mtumishi kuona jiji hilo linakuwa mfano wa kuigwa hapa nchini.
Ikumbukwe Eng. Hamsini kwasasa ni Mkurugenzi wa Tanga na hiki ni kikao chake cha kwqnza na watumishi wote wa Halmashaui hiyo akitokea Jiji la Arusha baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali mwezi Agosti 2024.
Comments
Post a Comment