JENGO LA DKT. SAMIA LILILO GHARIMU KIASI CHA SHILINGI BILIONI 9 LAKABIDHIWA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA.
SSH BUSINESS CENTRE KITUO KIKUU CHA KIBIASHARA JIJINI TANGA SASA NI MUDA WA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUJINAFASI.
Na Lucas Myovela - Tanga.
Halmashauri ya Jiji la Tanga imekabidhiwa rasmi jengo la kitega uchumi linalojulikana kama Dkt. Samia Suluhu Hassan Business Centre, lililopo katika Mji wa Kange Kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi baada ya ujenzi wa jengo hilo kukamilika na kuwa tayari kwa kutoa huduma.
Jengo hilo la kisasa ambalo limeungana na Kituo kikuu cha mabasi linasehemu mbalimbali za huduma za kijamii zikiwemo ofisi, Migahawa ya kisasa, Huduma za kibenki, Huduma za tikeketi, maduka ya kisasa makubwa na madogo, Kumbi za mikutano pamoja na Sherehe n.k limekabidhiwa jana Ijumaa Septemba 20, 2024.
Makabidhiano hayo yalifanywa kwa kusaini nyaraka kati ya Halmashauri, Mkandarasi aliyejenga jengo hilo, Mohammedi Builders Ltd, na Mtaalamu mshauri, QD Consultant (T) Ltd.
Ambapo kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la Tanga iliwakirishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Dkt. Stephen Mwandambo, ambaye aliongozana na Menejimenti ya Halmashauri wakati kwa Mkandarasi aliwakirishwa na Mhandisi Ammar Jasoowalla, na Mtaalam Mshauri akiwakilishwa na Meneja Mradi, Arch. Said Mwanga.
Jengo hilo lililowekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mnamo tarehe 22/04/2024 limegharimu kiasi cha shillingi Billion 9 fedha za Serikali Kuu ambapo ujenzi wake ulianza Julai 5, 2019, na ulikadiriwa kukamilika kwa kipindi cha miezi 12, lakini kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ya mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19, ujenzi ulichelewa na sasa tayari limekamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri hiyo.
Comments
Post a Comment