KISHINDO CHA TTCL :WILAYA ZOTE 139 KUFIKIWA NA MKONGO WA TAIFA

SASA NI MAWASILIONO YA HUAKIKA KWA WATANZANIA WOTE KUPITIA SHIRIKA LA TTCL.

Na Lucas Myovela -Arusha.

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limejinasibu kuwa wilaya 139 za Tanzania Bara hadi zitafikiwa na husuma ya mawasiliano kutia shirika hilo na hadi sasa tayari wamefanikiwa kuzifikia Wilaya 106 na kuziunganisha na Mkongo wa taifa wa mawasiliano.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha Mkurugenzi wa Ufundi na Undelezaji kutoka TTCL Mhandisi, Cecil Francis katika kongamano la Connect 2 Connect linalo fanyika Jijini humo kwa siku tatu lililo wakutanisha wadau mbalimbali wa mawasiliano wa ndani ya nchi na nje ya nchi ambalo limefunguliwa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa.


Mhandisi Cecil ameeleza kuwa wilaya 33 ambazo bado hazijafikiwa na mkongo wa Taifa wa mawasiliano utafikiwa hivi karibuni kati bajeti ya ilyopangwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 na serikali imeshatenga bajeti ya kwenda kukamilisha shughuli hiyo ili kuhakikisha wilaya zote zinaunganishwa na mkongo wa Taifa na zianze kupata huduma bora ya kimtandao na mawasiliano.

"Mkongo wa mawasiliano wa taifa ni kiungo kikuu cha mawasiliano ya sauti na Intaneti ambapo inaunganishwa na mikongo ya baharini ambayo inaleta Intaneti nchini.


“Mkongo wetu wa taifa wa mawasiliano ni kiungo kikuu cha mawasiliano ya sauti lakini vilevile na Intaneti na tunaunganisha na mikongo ya baharini ambayo inatuletea Intaneti hapa nchini na sisi pia tunaunganisha na nchi za jirani za Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi,Zambia na Malawi". Amesema Eng Cecil.


“Pia tumeshafanya maunganisho yamekwenda mpaka Msumbiji na tumeanza kuingia maunganisho yatakayofanya tuingie hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),kupitia Ziwa Tanganyika". aliongeza Eng. Cecil.

Aidha Eng. Cecil ameeleza kuwa shirika hilo linaendelea kuboresha maunganisho ya mkongo kwa kusogeza kwenye vituo vya baharini vilivyoko Mombasa nchini Kenya. Pia ameongeza kuwa shirika hilo kupitia mkongo wa taifa wa mawasiliano wamefanya kazi ya kuunganishwa kwa mawasiliano Mkoa kwa Mkoa na wilaya kwa wialaya.


“Sisi kama TTCL tukiwa kama chombo cha Serikali tumepewa dhamana ya kutoa huduma za mawasiliano hapa nchini na Kazi kubwa tuliyonayo TTCL ni kuhakikisha tunatoa mchango wa mawasiliano kwa mkongo tunao ujenga inafika kila sehemu ikiwa na ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kufikisha huduma kwa wananchi na kupunguza gharama za matumizi". ameeleza Eng. Cicil.



Comments