MTIFUANO MKALI MERERANI, TAHARUKI YA TANDA BAADA YA KIGOGO MMOJA KUPIGA SIMU NA KUTOA TAARIFA POTOFU.

🔻R.M.O AWASHIKIA CHINI AWAPA ONYO KALI WANAO KIUKA MAAMUZI YA KAMATI, AAPA KUWASHUGHULIKIA IPASAVYO.

🔻KAMATI YAANZA KAZI KWA KISHINDO YABAINI MAZITO YAAPA KUTO KUYUMBISHWA NA MANENO BALI KUSIMAMIA HAKI KWA WOTE.

Na Mwandishi wetu - MIRERANI.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usuluhishi na Usalama katika Migodi ya Tanzanite iliyopo katika Mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Charles Chilala amewataka wamiliki wa migodi hiyo kuheshimu maamuzi ya kamati pindi wanapoamua migogoro wa kuingiliana ndani ya migodi (Mitobozano) lengo likiwa ni kulinda amani na usalama mgodini.


Chilala alisema hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Njake Enterprises and Oil Transport inayechimba madini ya Tanzanite katika kitalu B Mirerani ,Japhet Lema kwa kuilalamikia kampuni ya Gem & Rock Venture mnamo mwezi septemba 02, 2024, wafanyakazi wa kampuni hiyo walilipua baruti pasipo makubaliano ya pande zote mbili kama ilivyo utaratibu na uchorongaji eneo lililositishwa na kamati kwa sababu maalum kitendo hivho kilipelekea  kuhatarisha amani kwa wafanyakazi wake na kuiomba kamati kuchukua hatua kali dhidi ya kampuni hiyo ya GEM & ROCK VENTURE.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema kamati iko kisheria na inatambulika na Wizara ya Madini hivyo aliwaomba wamiliki wa migodi kuheshimu maamuzi ya kamati vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria pindi wanapozarau maamuzi ya kamati.


"Meneja wa Gem & Rock Venture tulimuita ili kuzungumza nae na kisha aliitwa katika ofisi ya Wizara ya Madini Mirerani na kuonywa kuheshimu maamuzi ya kamati kwa kuwa kamati hiyo iko kisheria na wakiendelea kukaidi wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa mgodi wao". alisema Chilala.


"Kamati iligundua vitu vingi katika Mgogoro wa Njake na Gem & Rock na Kamati ilimwagiza meneja wa kampuni ya Gem & Rock watafute sehemu nyingine ya kufanyia kazi ambayo ni salama na pia kamati tumeamuru kampuni hiyo kuacha kufanya kazi katika eneo hilo hatua ambayo iliamuliwa na wajumbe nane kati ya tisa wa kamati hii". Alisisitiza Chilala.


"Tunataka amani na usalama katika migodi ya Tanzanite Mirerani hivyo kila mmiliki wa mgodi wa madini ya Tanzanite anapaswa kutii maagizo ya kamati ikiwa ni pamoja na kuwaagiza mameneja wao kufuata sheria na kanuni na sio vinginevyo". Alisisitiza Chilala


Naye Afisa Madini Mfawidhi wa Wizara ya Madini Mirerani, Nchagwa Chacha lalipoulizwa juu ya ukaidi uliofanywa na kampuni ya Gem & Rock Venture wa kudharau maamuzi ya kamati alisema kuwa suala hilo limemalizwa na maelekezo yameshatolewa kwa wahusika mengine yamebaki kwa taratibu za kiofisi.


Chacha aliwahimiza wamiliki wa migodi kuitambua na kuiheshimu kamati kwani imechaguliwa kisheria na iko kisheria hivyo wote wanapaswa kutii maamuzi yake ili uchimbaji wa madini ya Tanzanite ufanywe kwa kuzingatia sheria na kanuni kuepuka maafa yasiyokuwa ya lazima.


"Nikweli nimepokea taarifa hizo na tuliyo ufanya tulibaini kwamba taharuki iliyouwepo ni uzushi uliyo fanywa na kampuni ya Gem & Rock Vanture  nakulivyo fika katika mgodi wa Njake hatukuta kitu chochote kama alivyo kuwa ametoa taarifa.  Mimi nadhani huyu ni wakati sahihi wa wachimbaji kuchimba katika leseni zao na kuachana na migogoro isiyo ya lazima". Amesema Chacha.


"Lengo la Serikali ni kuweka ulinzi na miundombinu sahihi ya biashara kwa wawekezaji lengo ni kujenga taifa letu kiuchumi na kwa hapa mirerani propanganda ni nyingi niwakumbushe tu wachimbaji sheria zetu zipo wazi wazingatie hilo wasijishau na wafuate maagizo ma maamuzi wa kamati za usuluhisho wakishindwana huku huku sisi ni kuzifunga leseni zao". Aliongeza Chaha.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Njake Bw. Japhet Lema, amesema kuwa wafanyakazi wa kampuni ya Gem & Rock wamekuwa na tabia ya kukaidi maagizo ya kamati na kurudiarudia makosa yale yale hivyo aliomba kamati na ofisi ya Wizara ya Madini Mirerani kutoa makucha na kutoa adhabu stahiki ili tabia hiyo isiweze kujirudia tena.


Nae Mkurugenzi wa Gem & Rock Venture, Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti, alipo ulizwa na mwandishi wetu  juu taarifa hiyo ya kukaidi maamuzi ya kamati alisema sio kweli ila wafanyakazi wa Njake ndio waliovamia mgodi wake na kupora madini na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi na kusema kuwa taarifa zote anazo Chacha Afisa Mfawidhi Wizara ya Madini Mirerani lakini Chacha alipoulizwa alisema hakukuwa kitu kama hicho katika uchunguzi wao wa awali na kusema kuwa ulikuwa uzushi tu.


Pia Saitoti alipo ulizwa juu ya kulipua tena juu ya kulipua eneo hilo tarehe 2.9.2024 majira ya saa kumi na moja asubuhi ilihali kwamba eneo hilo lilikatazwa na kamati hiyo, Saitoti alisema kuwa yeye tayari kila kitu amekiwasilisha kwa RMO, na tulipo taka atupatie meneja wake ili kutoa uafanuzi huo alisema meneja wake yupo safari.


Jitihada zinaendelea kuutafuta uongozi wa Wizara wa madini kuanzia gazi ya katibu Mkuu wa Wizara pamoja na Waziri mwenye dhamana wa Wizara hiyo Mhe. Peter Mavunde ili kuendelea kupata ukweli zaidi juu ya chokochoko zinazo endelea katika machimbo hayo hayo ya madini adhimu duniani ya Tanzanite.

Moja ya Kipande cha Maamuzi ya kamati hiyo iliyowasilishwa kwa R.M.O.

Comments