🔴AWAREJESHEA KANISA KATOLIKI ARUSHA ENEO LAO NA FEDHA ZAO SHILINGI MILIONI 500.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa watendaji wote wa Serikalibkuanzia ngazi ya Mkoa hadi vijiji kutowaingilia wafugaji wote hapa nchini katika maeneo yao ya malisho kama ilivyo elezwa kwenye GN.
Aidha Rais Dkt. Samia amewarudishia kanisa katoliki Mkoani Arusha eneo lao walilokuwa wanalimiki kwa muda mrefu na bada uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Arusha na kisaha kuwataka kanisa katoliki kulipia eneo lao milioni 500 kitu ambacho Rais Samia ameutaka uongozi wa Mkoa kuresha eneo hilo pamoja na fedha walizo chukua.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI ) Mohamed Mtahengerwa wakati akiongea katika Mkutano wa hadhara Oktoba 4, 2024 Jijini Arushakuwa ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Machengerwa ameeleza kuwa katika kufuatilia kwake baadhi ya maeneo baada ya kutangaza vijiji ambavyo vitashiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa vijij vyote ni makazi ya wananchi pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kibinadamu yaheshimiwe kama alivyo elekeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Wapo miongoni mwetu watu wanaofanya kazi ya kumchonganisha rais na wananchi, naambiwa hapa arusha yapo maeneo ambayo viongozi waliyaweka kuwa mapori tengefu wakati ni maeneo ya malisho ya mifugo ya wananchi toka kizazi na kizazi hili haliwezekani maeneo ya wananchi na shughuli zao yabaki kama yalivyo na yaheshimiwe". Amesema Mchengerwa.
"Maelekezo yangu kwenu nikiwa kama waziri wa TAMISMI Rais ameridhia maeneo hayo yawe maeneo ya uchaguzi na wananchi waendelee kuishi na kufanya shughuli zao sitegemei kama kuna mtu chini yangu atakuwa na maelelezo mengine zaidi yangu, wapo watendaji huku chini wanakwenda kutengua kauli ya Rais kuwaondoa wananchi, Mimi ni Waziri wa tofauti endapo nikibaini viongozi wote wa eneo hilo nitawafuta kazi mara moja". Ameongeza Mchengerwa.
Aidha Mchengerwa ametoa ufafanuzi juu ya eneo la kanisa katoliki walilokuwa wakimiliki kwa siku nyingi na wakanyang'anywa na badae wakatakiwa kulinunua tena na wala eneo hilo halikuwa la serikali ila viongozi waliyokuwepo walikubali kupokea fedha ambazo hawakustahili.
"Jana nimezungumza na Mhe. Rais Samia kumueleza jambo hili na akanambia kwamba, Niwaelekeze Mkoa pamoja na Jiji kuwa eneo hilo lilejeshwe haraka kanisa mara moja na fedha hizo Milioni 500 zilejeshwe kanisani mara moja". Amesema Mchengerwa.
"Nawaelekeza nyinyi Mkoa chini yako Rc Paul Makonda mzirejeshe fedha hizo kwa namna mlivyo zichukua mwanzo na njia hiyo hiyo zirudi kanisani hayo ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia". Amesema Mchengerwa.
Aidha katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amelidhishwa na miradi mbalimbali na utekelezaji wake katika Halmashauri ya Jiji la Arusha inayoendelezwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasan, ambapo zaidi ya Trilioni 1 zimepokelewa katka halmashauri hiyo.
"Leo nimeona mradi wa hosptali ya wilaya inayojengwa na jiji la Arusha inajengwa kwa zaidi ya Bilioni 17 niwapongeze sana jiji la Arusha, Jitahidini viwango vya hosptali hii viwe vya kimataifa kama ilivyo kusudiwa na wageni wetu wanapokuja wapate huduma stahiki". Amesema Mchengerwa.
"Ilikuiga Arusha kuzidi kuwa Mji wa kitalii nakuelekeza Meneja mkuu tarura anza na km 6 za barabara ya lami hapa Arusha kuanzia sasa kaangalie maeneo ya kimkakati ili muweza kuwajengea wananchi hawa miundombinu bora na wao waweze kukuza uchumi". Amesema Mtengerwa.
"Niwaombe wakuu wa wilaya wote hapa nchini kuendelea kuwa wabunifu kama alivyo Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kujenga vivutio mbalimbali kwa wageni hasa kwa kutosahau huduma za afya". Amesisitiza Mtengerwa.
"Ujenzi wa taifa letu ilijengwa na kuhasisiwa na Baba yetu wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na viongozi wengine waliyofuatia na sasa dhima hiyo inaendelezwa na Dkt Samia, na Arusha tulichelewa kwa siasa za maji taka na leo hii wamebaki kugaragara kwenye mitandaoni". Amesema Mchengerwa.
"Nitake nikwambie Makonda chapa kazi hiindiyo kazi Rais Samia aliye kutuma Arusha, Kama ni Spana piga spana achana na siasa za majitaka na mimi kama waziri wako nakuamini sana na nipo nyuma yako kuhakikisha Arusha inasonga mbele". Amesema Chengerwa.
Hospital iliyojengwa iko pande ipi hapa Jijini?
ReplyDelete