WAZIRI MHAGAMA ATOA MAELEKEZO KWA WATAALAMU WA AFYA NA LISHE PAMOJA NA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUTEKELEZA MAMBO HAYA..
🔴AWATADHALISHA WANANCHI KUZINGATIA LISHE BORA KWA USTAWI WA TAIFA.
🔴AWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA LISHE ILI KUKABILIANA NA UTAPIA MLO WA AINA ZOTE.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Waziri wa Afya Nchini Tanzania Jenista Mhagama amewataka watanzania kuzingatia mlo kamili ili kukabiliana na utapia mlo katika jamii zao wanazoishi kitu ambacho kwasasa ni tishio kwa taifa.
Aidha amewaomba wadau wote wa sekta ya Afya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuimarisha utoaji wa huduma za lishe ili kakabiliana na utapia mlo wa aina zote katika nchi ya Tanzania na kuwataka wataalamu wa Afya kutekeleza mambo ya muhimu yanayo husu lishe katika jamii.
Waziri Mhagama ameeleza kuwa katika kuzingatia mlo kamili na watanzania wawe na afya bora wataalamu wa Afya pamoja na lishe wanapaswa kufanya majukumu yao ya utoaji elimu kwa jamii kama ilivyo elekezwa.
"Niwakumbushe watalaam wetu wa Afya na Lishe katika ngazi zote kuhakikisha kuwa kila mmoja Kutoa elimu ikiwemo uhamasishaji jamii kuhusu ulaji unaofaa na matumizi ya vyakula vilivyoongezwa virutubishi kupitia majukwaa mbalimbali". Amesema Mhagama.
"Kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa afua za Lishe katika ngazi zote, ili kuhakikisha afua hizi muhimu zinatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na Taratibu zilizopo". Ameongeza Mhagama.
"Halmashauri zote Nchini kuhakikisha kuwa fedha za kutekeleza afua zote za Lishe ikiwemo uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula, uhamasishaji na elimu ya lishe kwa jamii na tathmini ya hali ya Lishe ili kubaini matatizo ya utapiamlo; zinatumika kama ilivyokusudiwa". Amesisitiza Mhagama.
"Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa yalianza kuadhimishwa tangu mwaka 2020 yakiwa na kaulimbiu isemayo "Lishe bora ni kinga dhidi ya magonjwa", na kaulimbiu ya mwaka huu inasema "Mchongo Ni Afya Yako, Zingatia Unachokula", Kaulimbiu hii inatukumbusha kuwa afya bora ni nguzo muhimu ya afya ya mwanadamu". Amesema Mhagama.
"Jamii bado inakabaliwa na changamoto ya utapiamlo wa aina zote tatu unaojumuisha Utapiamlo wa Lishe pungufu ikiwemo udumavu, ukondefu, uzito pungufu hususani kwa watoto, Utapiamlo wa upungufu wa vitaminini na madini mwilini yaani njaa iliyofichika ikiwemo upungufu wa damu, pamoja na Utapiamlo wa Lishe ya kuzidi unaoambatana na uzito uliozidi au kiribatumbo pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu". Ameongeza Mhagama.
"Utapiamlo hudhoofisha makuzi ya watoto kimwili na kiakili, huongeza hatari ya magonjwa na gharama kubwa za matibabu, na huathiri ubunifu na uwezo wa kufanya maamuzi wakati wa utu uzima. Vilevile, utapiamlo hupunguza tija na uzalishaji mali, hivyo ni kikwazo kikubwa katika ustawi wa jamii na maendeleo kiuchumi kwa mtu mmojamoja, kaya, jamii na Taifa kwa ujumla". Amesisitiza Mhagama.
"Inatupasa kuchukua hatua ya makusudi kwa kuwa makini na kufanya uamuzi sahihi kila siku kuhusu aina na ubora wa vyakula tunavyokula au kuwalisha watoto wetu na nimuhimu kula mlo kamili wenye mchanganyiko wa vyakula mbalimbali binavyo patikana katika mazingira yetu". Amesisitiza zaidi Mhagama.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni " MCHONGO NI AFYA YAKO ZINGATIA UNACHO KULA".
Nukuu: "Ulaji wa vyakulamchanganyiko ni Msingi wa Afya bora, hivyo Tuzingatie Tunachokula".
Comments
Post a Comment