🔻BALOZI CHANA WAIPONGEZA TFS KUVUKA MALENGO KATIKA MAKUSANYO YA SERIKALI.
🔻ATAKA MASLAHI BORA KWA MAKAMANDA ILI KUBORESHA UTENDAJI KAZI.
Na Lucas Myovela- Arusha.
Aidha ameitaka manejimenti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuwathibitisha watumishi wenye sifa ambao wamekaimu nafasi hizo kwa muda mrefu, ili kuongeza ufanisi.
Balozi, Chana ameyasema leo Novemba 05,2024 Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa Makamanda waWakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Balozi Chana ameeleza kuwa malengo waliyovuka ya kukusnaya mapato ya shilingi Bilioni 166 sawa na asilimia 103 kama wangekuwa wanatumia mfumo wa TEHAMA malengo hayo yangekuwa makubwa zaidi kuliko ilivyo sasa.
"Upo ushahidi kabisa kwamba matumizisahihi ya mifumo ya TEHAMA inasaidia kuboresha kazi, utawala bora na kupunguza vitendo vya rushwa ambavyo vingeweza kujitokeza, kuimarisha makusanyo na kudhibiti matumizi ya maduhuli ya serikali". Ameeleza Balozi Chana.
Pamoja na kuipongeza TFS Balozi, Chana ameeleza kuwa kwa sasa taasisi nyingi za serikali hukusanya mapato kwa mfumo wa TEHAMA kwa lengo la kuzifanya fedha za serikali kuwa salama na kukusanya mapato zaidi na kutokuwa na urahisi wa kuchezewa na watumishi wasiyokuwa waaminifu na waadilifu kwatika ujenzi wa taifa.
"Hadi mwezi Juni mwaka huu TFS mmekusanya zaidi ya shilingi Bilioni 166 na kuvuka malengo yaliyokusudiwa hivyo pongezi za dhati kwa menejimenti chini ya Kamishina Silayo na Bodi lakini jitihada za ziada zinahitahija katika ukusanyaji mapato kama nilivyo waelekeza". Ameelez Balozi Chana.
''Ninakuomba Kamishina sasa mnapaswa kubadilika na kukusanya mapato kwa mfumo wa TEHAMA ili mapato yawe mengi na salama na malengo yaliyokusudiwa yazidi kupaa kwa asilimia zaidi ya mia moja''. Ameongeza Balozi Chana
Akizungumzia uadilifu katika Kazi, Balozi, Dkt.Chana aliwataka Makamanda wa TFS kufanya kazi kama Makanda wa Jeshi kama ilivyo katika mfumo wa uendeshaji Kiraia ikiwa ni pamoja na kuwa wazalendo katika kazi na kufuata kanuni na sheria za taasisi.
"Sifa kuu ya askari kwanza ni kuwa mzalendo, muadilifu na muaminifu hivyo Makamanda wa TFS mnapaswa kwenda sambamba na misingi hiyo ili kulinda kanuni za kazi katika uendeshaji wa shughuli zenu ili serikali iendelee kuwaamini zaidi". Amesema Balozi Chana.
"TFS mnapaswa kufanya kazi kisasa ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kununuwa vitendea kazi vya kisasa ikiwa ni pamoja na magari ya kisasa,ndege na helkopta vyote vinahitajika katika utendaji kati katika misitu yetu hapa nchini ikiwa nipamoja na kuwa na ulinzi ndani ya misitu". Ameongeza Balozi Chana
"Niwaombe menejimenti na Bodi ya TFS kuhakikisha mnatatua changamoto za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapandisha vyeo wanapostahili na kuongezewa maslahi kwa wakati. Pia niwataeke Makanda na watumishi wote kuhakikisha mnafikisha changamoto zenu mahali sahihi nasiyo kuongelea vibarazani huko kunaharibu nidhamu kazini". Amesisitiza Balozi Chana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TFS, Brigedia Jeneral Mbaraka Naziad Mkeremy alisema kuwa TFS imejipanga kuhakikisha malengo ya makusanyo ya kila mwaka yanafikiwa na kuzidi ili taasisi hiyo iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi na kuhakikisha taasisi hiyo inatatua changamoto za jamii.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi, Mhandisi Enock Nyanda ambaye ni mjumbe wa Bodi ya TFS alisema kuwa Bodi kwa kushirikiana na menejimenti imekuwa ikishirikiana katika kuhakikisha inajali maslahi ya wafanyakazi na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mwenyekiti wa Bodi alisema kuwa TFS imekuwa ikishirikiana na jamii katika kutatua changamoto lengo ni kutaka jamii kuishi kwa kufata kanuni na sheria za misitu na nyuki.
Awali, Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof. Dossantos Silayo amesema lengo la kikao hicho ni kujengeana uwezo wa utendaji kazi, kubadilisha uzoefu,kujadiliana na kushauriana kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za utendaji kazi ili kuimarisha mifumo ya utendaji kazi.
Comments
Post a Comment