MKURUNGENZI AWAPIGA MARUFUKU WENYEVITI WALIYO CHAGULIWA KUUZA MAENEO KIHOLELA NA KUFANYA MAAMUZI YA KIBABE KWA WANANCHI NA KUWANYANYULIA MABEGA.

🔻AWATAKA WAKAHUDUMIE WANANCHI NA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO.


🔻WENYEVITI 924 PAMOJA NA WAJUMBE WAO WAAPISHWA RASMI ARUSHA.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Wenyeviti wa wamitaa pamoja na wajumbe wa makundi yote leo wamekula kiapo rasmi kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi baada ya kuchaguliwa hapo jana Novemba 27, 2024 katika uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa.


Jumla ya viongozi hao wa mitaa 924 walikula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya mwanzo Arusha mjini Salma Athumani Mwamende ni wenyeviti wa mitaa 154 wa jiji la Ausha, wajumbe wa wananwake 308 na wajumbe kundi mchanganyiko 462.

Mara baada ya viongozi hao kula kiapo hicho Mkurugenzi wa jiji la Arusha John Kayombo alipata wahasa na kuwapa nasaha viongozi hao wa Serikali za mitaa waliyopata nafasi ya kuongoza wananchi kwa kipindi cha miaka 5 hadi mwaka 2029 kutokujihushwa na maamuzi ya kibabe ya kuuza ardhi kiholela.


Kayombo ameeleza kuwa wananchi wanaimani kubwa na serikali yao na wao kama viongozi waliyo aminiwa wasiwe chanzo cha kuivuruga amani hiyo maana Rais Dkt. Samia amesha paleka fedha za maendeleo pamoja na fedha za makundi maalumu na kuwataka wakasimamie ipasavyo miradi hiyo na wasiwe chanzo cha migogoro.

"Mmepata nafasi hii adhinimu mliyo aminiwa na wananchi, Sitaki kusikia nyie ndiyo chanzo cha migorogoro, Mmetoka huko katika vyama vyenu sasa mpo chini yangu, Ninataka mkawe chachu ya utatuzi wa changamoto za wananchi". Amesema Kayombo.


"Nataka mkasimamie vyema ulinzi na usalama katika maeneo yenu kiwe kipaumbele chenu namba moja maana Arusha ni Kitovu cha utalii, Ulinzi ukiimalika uchumi utapanda na jiji litakuwa salama kwa wageni". Ameongeza Kayombo.

Aidha kayombo amepiga marufuku ujenzi holela ili kulinusuru Jiji la Arusha kubaki salama pia amewataka viongozi hao kutokwenda kunyanyua mabenga na kuwasumbua wananchi.


Pia Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa atawapa semina ya siku mbili viongozi hao ili kuweza kujua miongozo ya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa weledi mkubwa pamoja na kuwapa vifaa vya kisasa.










Comments