🔻AWATAKA KUKWEPA RUSHWA KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Mussa Misaile ametoa kauli hiyo mapema leo Novemba 17,2024, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa manunuzi yanayoendelea Jijini Arusha
Mafunzo hayo yameandaliwa na bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) kwa kushirikisha wataalamu wa sekta hiyo toka halmashauri zote na sekretarieti ya mkoa wa Arusha.
Miseile amewataka kujiepusha na vitendo vya rushwa na kujikita zaidi katika kusimamia kikamilifu fedha zote za umma zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali.
"hakikisheni mnajifunza kwa umakini mkubwa kuandaa na kutunza mikataba,na mzingatie yaleyote mnayofunzishwa hapa ili mkitoka muende mkayatekeleze kwa vitendo". Amesema Misaile.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi hapa nchini (PSPTB) Godfred Mbanyi alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu hao juu ya sheria mpya ya ununuzi na namna ya kusimamia mikataba.
Ameeleza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika maeneo mengi hapa nchini ni wataalamu wa ununuzi kufanya kazi pasipo kusajiliwa na bodi hyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria na kuwataka wale wote ambao hawajasajiliwa wajisajili mara moja.
"Natoa wito kuzingatia sheria kanuni na taratibu za manunuzi katika kutekeleza majukumu yenu,na nawataka wale wote ambao hawajasajiliwa na bodi kujisajili haraka iwezekanavyo kwani iko kwa mujibu wa sheria na anayefanya kazi bila kusajiliwa anavunja sheria za nchi".Amesema Mbanyi.
Comments
Post a Comment