WIZARA YA MADINI YAWEKA HISTORIA MPYA DUNIANI

"TUNAWEZA KUVUKA MALENGO". 

Wizara ya Madini imeweka historia ya kukusanya mapato nchini kutoka katika vyanzo vyake kwani katika kipindi cha miezi mitano tu cha kuanzia julai mwaka huu hadi Disemba mosi imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 434.


Hayo yalisemwa na Waziri wa Madini,Antony Mavunde kabla ya kuzindua mnada wa madini ya vito na kusema kuwa hadi kufikia Disemba 31 mwaka huu wanataka kukamilisha makusanyo na kufikia shilingi Bilioni 500.


Mavunde alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25 malengo ya Wizara ni kukusanya zaidi ya shilingi Trilioni moja na huenda malengo hayo yakavukwa kwa kuwa watendaji wa Wizara hiyo wako makini katika kuitumika nchi.


Alisema Wizara ya Madini ni Wizara nyeti na serikali inategemea katika kuendesha uchumi wa nchi na makusanya katika Wizara hiyo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kwani katika kipindi cha mwaka 2015/16 Wizara ya Madini ilifanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 161


Waziri Mavunde alisema katika mwaka wa fedha 2023/24 Wizara ya Madini ilikusanya zaidi ya shilingi Bilioni 753 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya maduhuli na kuonyesha wazi kuwa sekta hiyo ikisimamiwa vizuri na watendaji kufanya shughuli zao kwa uadilifu na uaminifu sekta hiyo ni moja ya muhimili mkubwa wa serikali katika kuongeza mapato.


Alisema katika kuboresha sekta hiyo ya madini katika kitengo cha makusanyo Wizara ya Madini imejipanga kikamilifu ikiwa ni pamoja na kurudisha minada na maonyesha ya madini ya vito ya Kifaifa na Kimataifa ili wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo wa ndani na nje waweze kunufaika katika minada hiyo na serikali iweze kupata mapato.


Waziri Mavunde alisema urejeshaji wa minada ya vito nchini ni jitihada za serikali kutaka ushirikishwaji kwa wachimbaji na serikali ili kufanya shughuli za uchimbaji na biashara ya sekta ya madini kwa uwazi na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.


Alisema minada yote itakuwa ikifanywa kwa njia ya elekronic ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa njia ya uwazi na uwepo ya minada hiyo ni chachu ya maendeleo kote nchini hivyo aliwaondoa shaka wachimbaji kuwa hakuna atayeporwa madini yake na serikali.


''Minada yote itafanywa kwa njia ya kielekronic lengo ni kutaka kuona kila kitu kinafanywa kwa uwazi na ukweli na wenye kununuwa madini ya vito wanunuwe kwa njia ya haki bila ya kuwa na upendeleo wowote''alisema Mavunde


Akizungumzia Mnada wa Madini ya vito ya Mirerani ambayo mengi yalikuwa madini ya Tanzanite ,Waziri Mvunde alisema thamani ya madini yaliyouzwa jana ni zaidi ya shilingi bilioni 3 yenye uzito wa gramu 1284.60 na amewashukuru wafanyabiashara wa madini wakubwa kwa wadogo kwa kujitokeza katika mnada huo.


Waziri Mvunde alisema kuwa serikali iko katika mkakati madhubuti ya kurejesha hadhi ya madini ya viyo ya Tanzanite ili jiwe hilo liwe na thamani kubwa nyakati zote kitaifa na kimataifa hivyo aliwataka wafanyabiashara wa sekta hiyo kushirikiana na serikali katika kufanikisha hilo.


Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,Kirumbe Nyenda alimpongeza Waziri wa Madini kwa kuwa na ushirikiano wa kutosha na kamati hiyo na kuifanya Wizara hiyo kuendelea kupaa katika ukusanyaji mapato ya serikali.


Nyenda alisema pamoja na hayo pia alimshukuru Mavunde kwa kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa wachimbaji wakuwa kwa wadogo na kuonyesha wazi kuwa biashara katika sekta hiyo inafanywa kwa kufuata sheria.


''Tunaiomba Wizara ya Madini iendelee kujipanga kikamilifu katika kuiongozea mapato serikali na kutatua changamoto zote za wachimbaji nchini ili shughuli za uchimbaji na biashara zifanywe kwa umakini wenye kufuata sheria zilizowekwa''alisema 


Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Qunne Sendiga mbali ya kumshukuru kurudisha minada kote nchini hususani katika Mji wa Mirerani pia alimwomba Waziri Mvunde kuhakikisha anasimamia umaliziaji wa jengo la soko la madini lililopo Mirerani.


Alisema jengo la Tanzanite Tower lililojengwa katika Mji wa Mirerani linagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.4 na Mkandarasi ametishia kujitoa kwani amekuwa halipwi fedha kwa wakati hatua ambayo Waziri alijibu kuwa suala hilo atalishughulikia haraka iwezekanavyo.


Ujenzi wa sokol la Tanzanite Mirerani ulianza mei 2022 na ilitarajiwa kukamilika mei 2023 na ghamara za ujenzi huo ilikuwa zaidi ya shilingi Bilioni 5.4 ambao ni maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka mji wa Mirerani unanufaishwa na Madini hayo kama ilivyokuwa Mji wa Geita unavyonufanishwa na madini ya dhahabu.


Sendiga alimkumbusha Waziri juu ya ujenzi wa Zahanati ndani ya ukuta wa Mirerani na ukarabati wa barabara vyote Waziri Mavunde aliahidi kuyafuatilia ili miradi hiyo iweze kuanza na kufanya kazi kwani ni moja ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi{CCM}.


Naye Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka yeye alimpongeza Mvunde kwa kurudisha mnada wa Tanzanite Mirerani ndani ya ukuta na kuwataka wale wote wenye njia potofu ya kutaka mnada wa madini ya vito ya Tanzanite kufanyika nje ya Mirerani hawataweza kwani agizo hilo ni la Rais na hakuna mwingine anayepindisha.


Sendeka alimtaka Waziri Mavunde kutatua changamoto ya upekuzi katika geti la Magufuli ndani ya ukuta wa Mirerani na kusema kuwa kinachofanyika sasa nio sahihi kwani wachimbaji wanatoka migodini mapema lakini wanapekuliwa hadi usiku wa sasa 8 usiku.
























Comments