ATAKA HALMASHAURI HIYO KUFANYA UWEKEZAJI WA HOTEL YA KISASA NA KUMBI ZA MIKUTANO ILI KUONGEZA MAPATO.
Na Lucas Myovea -Arusha.
Mhe. Makonda amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa kuwa mradi huo umekuwa ukisuasua bila sababu za msingi ilihali tayari Rais Samia Suluhu Hassan alikwisha idhinisha zaidi ya Bilioni 6 za ujenzi wa awamu ya pili ya Jengo hilo la Ghorofa sita, Akitaka pia taratibu za kimkataba na Ujenzi kwa awamu ya tatu kuanza kuandaliwa haraka badala ya kusubiri kukamilika kwa ujenzi awamu ya pili.
Pia wameahidi kushirikiana na Wataalamu na Watendaji wengine katika kusimamia kikamilifu maelekezo ya Mhe. Paul Christian Makonda ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na Ujenzi wa Jengo hilo haraka iwezekanavyo.
JIJI LA ARUSHA LATAKIWA KUWEKEZA KWENYE KUMBI ZA KISASA ZA MIKUTANO.
Akisisitiza umuhimu wa kuacha alama katika Uongozi, Mhe. Makonda amesema Ujenzi wa Kumbi hizo za mikutano si tu utasaidia kuingiza mapato kwa Halmashauri, bali pia kuunga Mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuifanya Arusha kuwa ya utalii wa Mikutano, michezo na utalii wa mbugani.
Aidha Mhe. Makonda amewataka Viongozi mbalimbali ngazi za Halmashauri kuendelea kuhamasisha wananchi na wawekezaji mbalimbali kuwekeza kwenye ujenzi wa kumbi za mikutano na hoteli, akisema Mkoa wa Arusha bado una uhitaji mkubwa wa masuala hayo kutokana na mahitaji makubwa yanayotokana na mikutano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa inayofanyika Mkoani Arusha.
Comments
Post a Comment