CHUO CHA UHASIBU ARUSHA (IAA) CHA NG'ARA KWENYE MASHINDANO YA CYBER CHAMPIONS YA MWAKA 2025.
By: Lucas Myovela.Mashindano hayo adhimu ya kusaka vijapaji kwa vijana katika nyanja ya Tehama yameandaliwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Aidha Chuo cha IAA kimefanikiwa kutoa washindi saba (07) katika washindi kumi (10) bora (Top Ten) wa mashindano hayo na kuzidi kuonyesha uhimara wake wa kufua vijana katika nyanja ya kimtandao ambapo kwasasa ndipo dunia inaelekea na kuweza kupunguza wimbi la ajira nchini na kuzalisha wataalam bora wenye uwezo wa kitaifa na kimataifa.
“Kwa sasa Chuo tumewekeza katika miundombinu ya TEHAMA, mitaala na rasilimaliwatu, IAA kupitia Mradi tuliyo nao wa HEET tunajenga kituo kikubwa cha umahiri cha TEHAMA, ambapo mtu yeyote atakayehitaji suluhisho la changamoto yoyote ya TEHAMA atakuja IAA na kupata ufumbuzi".amesema Prof, Sedoyeka.
Comments
Post a Comment