SASA NI MAKAMPUNI YOTE YA SIMU KUTUMIA NAMBA 100 KUWASILIANA NA WATEJA WAO.Na Lucas Myovela - Arusha.
"kampeni hii ya pamoja ni mkakati wa serikali na kampuni za simu kutoa elimu kwa umma kupitia jumbe mbalimbali zitakazotumwa kwa wamiliki wa simu kupitia kampuni mbalimbali ili kuepuka utapeli kutoka kwa matapeli wanaorubuni wananchi kupitia simu za kiganjani". Mesema Silaa
Aidha Silaa ameeleza kuwa kikao hicho cha wadau wa mawasiliano ya simu kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imelenga kuhakikisha kampeni hiyo ya sitapeliki inalengo la kutoa elimu kwa jamii katika kushughulikia utapeli huo mtandaoni huku akinukuu jumbe chache zitakazotumwa kwa wananchi kupitia simu zao
"Ni vema kulinda taarifa zako kwa kutumia nywila sahihi na tofauti kwa kila akaunti ikiwemo namba, Alamance, herufi kubwa na ndogo, usifuate maelekezo au kutoa neno la siri(nywila) kwa mtu yoyote, linda taarifa zako kwakuepuka kubofya viungajlnishi usizovifahamu, uhakiki wa namba ya simu kupitia*106# kisha chagua kuona namba zilizosajiliwa na NIDA". Ameeleza Silaa.
Pia ujumbe mwingine ni kukumbushwa mtoa huduma atawasiliana na wataje wake kupitia namba 100 pekee na kama si namba 100 usitoe taarifa zako huku ujumbe wa sita ni usiruhusu utapeli au ulaghai wa simu au ulaghai wa simu.
Silaa amesisitiza kuwa kwa sasa serikali haijapokea taarifa za udukuzi wa mawasiliano kutoka kwa wateja ikiwemo kutumia mtandao kwa usahihi huku akisisitiza kampuni za simu kutoa elimu kwa wateja huku jeshi la polisi na TCRA waendelee kudhibiti matukio ya kiulaghai kupitia mitandao ya simu ikiwemo kuathiri mifumo ya kifedha kupitia kidigiti.
Comments
Post a Comment