JAJI MUGETA ATAKA MABADILIKO KATIKA TAASISI ZA HAKI MADAI NA JINAI KUZINGATIA WELEDI KATIKA UTOAJI WA HAKI.
Na Lucas Myovela - Arusha.
"Taasisi hizi ni muhimu kuzingatia Sheria,kanuni na taratibu za kisheria katika utekelezaji wa majukumu na kuhakikisha upatikanaji wa haki bora na kwa wakati kwa watanzania". Alisema Mgeta.
"Ukimuuliza mtanzania yoyote anataka nini kwenye taasisi za haki madai, atakuambia anataka huduma bora, ya haraka na kwa heshima, ndio hitaji lake na hapo ndio mtihani ulipo katika miaka 25 ijayo tutakidhi vipi mahitaji hayo mbele ya wananchi bila kubadilika". Amesisitiza Jaji Mgeta.
Jaji Mugeta ameyasema hayo February 3.2025, katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini, Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kikanda katika Mkoani Arusha katika viwanja vya mahakama kuu Arusha na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali.
Mugeta ameeleza kuwa mabadiliko yanayohitajika katika taasisi zinazohusika na haki ni kuvaa jukumu la kuelimisha jamii kuhusu haki zao pamoja na Sheria zinazowalinda ili kuwapa uwezo wa kudai haki zao pindi wanapo ona zinataka kupotea dhidi ya watu wenyenia ovu.
"Niwaombe wote mnao husika na taasisi hizi muweze kuweka mifumo imara ya kisheria ya utoaji huduma ndani ya kila taasisi tena iliyo thabiti na wa haki kwa uwazi unao eleweka ili kuepusha matumizi ya utashi kwenye kufanya maamuzi kwa wananchi". Ameongeza Mugeta.
"Haya ni mambo ya msingi katika maendeleo ya dira na kamwe tusiendelee kudhani utoaji wa haki si sehemu ya maendeleo endelevu, Kwani haki ndio msingi wa maendeleo" amesema na kuongeza, Haki inayopatikana kwa wakati hupunguza migogoro na kuachilia rasilimali zilizofungwa ili ziingie kwenye mnyororo wa uzalishaji mali". Amesisitiza Jaji Mugeta.
Aidha Jaji Mugeta ameeleza kuwa kuwa katika rasimu ya dira ya taifa ya mwaka 2050 inataka kuwe na Taifa moja kama Jamhuri ya Muungano yenye jamii inayothamini utu, haki, Uhuru na Demokrasia na Taifa ambalo linasimamia rasilimali za nchi na kuimarisha utamaduni na tunu za Taifa.
"Katika kuyafikia haya, taasisi za haki madai zitahusika kusimamia eneo la utawala Bora, haki jamii, Uhuru na Demokrasia, tena wenye ufanisi katika kutazama haki za binadamu na usawa mbele za Sheria sambamba na usawa mbele ya utoaji haki madai kwa wananchi Ili kufikia jamii isiyo na vurugu wala ukatili" amesema na kuongeza.
"Nimesema hivyo ili kufikia dira yetu ya taifa lazima haki na wajibu viende pamoja na hii ni katika pande zote sio unakuta taasisi ya umma inadaiwa na mteja amekuja kulalamika lakini unaambiwa huruhusiwi kukamata mali fulani ni ya umma, hatuwezi kufikia huko tunakotaka" Ameeleza Njooka.
Aidha katika maadhimisho haya ya wiki ya sheria kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Comments
Post a Comment