WAZIRI SILAA AWATAKA WANAHABARI, WASANII NA WATU MASHUHURI KUUNGANA KATIKA KAMPENI YA "SITAPELIKI"

AAPA KUWANYOOSHA MATAPELI KUELEKEA UCHUMI WA KIMTANDAO.

ASEMA MPAKA SASA LINE ZA SIMU NI MILIONI 86.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amewataka wanatasnia ya habari bapa nchi na watu wengine mashuhuri kuungana kwa pamoja katika kampeni ya  "Sitapeliki" ili kuwafikia watanzania wengi kupiga vita matapeli wa mitandaoni.

Waziri Silaa ameyasema hayo mapema leo February 21,2025 alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Arusha.


"Niwaombe wanahabari wote nchini, wasanii na watu wote mashuhuri tuungane kwa pamoja katik kmpeni hii ya "sitapeliki" ili kuweza kumaliza wimbi la utapeli katika nchi yetu nina imani kila mtanzania akiwa mlinzi wa simu yake na kuto kutoa siri za akaunti yake tutaweza kupiga hatua kubwa". Amesema Silaa.

"Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anayo malengo maubwa ya kuikuza sekta ya hii ya mawasiliano na kampeni hii ni endelevu kuelekea malengo ya uchumi wa kimtandao ambayo dira yake ni miaka 10 ambapo Mhe. Rais aelizindua mwaka 2024 hadi 2034, Hivyo basi kila mtu anaye miliki hata kundi la Whatsap aweze kupaza sauti na kushirikisha wafuasi wake jumbe mbalimbali za "Sitapeleki". Ameongeza Silaa.


"Niwaombe sana watanzania kuweka namba za siri ambazo hagatani ili kuepusha kuibiwa fedha zao mtandaoni, Pia wasiwe wepesi kutoa taarifa pindi wanapo pigiwa simu na watu wasiyo wajua kwasasa ukipigiwa aimu mtu akajitambulisha ametoka mtandao furani na namba ya kaida mripo haraka sana ili aweze kufuatiliwa". Ameongeza Silaa.


Aidha katika hatua nyingine Waziri Silaa ameelezea mwenendo na ukuaji wa mawasiliano hapa nchini ambapo kwa sasa nchi nzima imweza kugikiwa na mawasiliano na uboeshaji wa mkongo wa taifa ukielekea kukamilika na kupunguza changamoto kadhaa za kimtandao.


"Kwasa kwa Tanzania kuna line za simu milioni  themanini na sita na laki nane ( 86,800,000) ambazo zinatumika hii inaonyesha mashirikiano mazuri ya serikali na taasisi za mawasiliano". Amesema Silaa.


Ameeleza kuwa mbali na kuwa na changamoto uboreshaji bado unaendelea kwa kushirikiana na wadau wote wa mawasiliano pamoja na vyombo mbalimbali vya kimamlaka ili kuweza kuifikia dira ya mafanikio.


Kampeni hiyo ya "Sitapeliki " imezinduliwa jana Jiji ni Arusha na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Jerry Silaa ili kudhibiti wizi mtandaoni kupitia simu za mikononi kwa wananchi wanaopiga matapeli kupitia namba zisizotambulika


Kwasasa namba zitakazo tumika kwa nchi nchi nzima kuwasiliana na mteja kutoka kwa mtoa huduma ni 100 pekee na namba ya kuripoti tukio la kupigiwa simu na matapeli ni 15040 na namba ya kuangali namba yako ya NIDA imesajili line ngapi ni *106#.



Comments