DKT SAMIA ATEKELEZA KWA VITENDO AZIMIO LA BEIJING.

🔻SASA WANAWAKE KUWA NA HAKI ZA KIJINSI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Waziri wa Ulinzi Dk. Stegomena Tax, ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza kwa vitendo azimio la Beijing la haki za wanawake na Kijinisia kwa kutoa fursa kwa wanawake kupata nafasi mbalimbali katika ngazi na maamuzi na uongozi.

Aidha amesema Rais,Dk, Samia amewakwamua wanawake katika sekta mbalimbali kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo hasa inayogusa maisha ya kila siku ya wanawake inatekelezwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo fursa za kuwakwamua wanawake kiuchumi.


Dk,Stegomena alisema hayo jana Jijini Arusha wakati akifungua kongamano kongamano la wanawake Kanda ya Kaskazini lenye kauli mbiu ya Ushiriki wa Wanawake katika Utalii ,Mali Asili katika miaka 30 ya Beijing.


"Tanzania imetoa msukumo mkubwa wa ulingo wa Beijing ambapo tumefanikiwa kuwa na Rais mwanamke ambaye amechukia hatua madhubiti kihakikisha wanwake wanajikwamua na kupata nafasi katika ngazi za maamuzi na uongozi".


Kuhusu Sekta ya utalii Dk,Stegomena Tax alisema Rais Dk,Samia amefanya kazi kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia filamu ya The Royal Tour ambayo imepngeza idadi ya watalii wanaokuja hapa nchini na kuchagiq ongezeko la ajira katika sekta hiyo.


"Sekta ya utalii hapa nchini imetoa ajira milioni 1.5 na katika ajira hizo asilimia 60 ni wanawake lakini licha ya mafanikio hayo bado kuna changamoto zinazowakabili wanawake hao ambapo asilimia 40 wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo kutopewa fursa sawa".


Alisema kutokana na changamoto zilizopo katika sekta ya utalii serikali imefanya maboresho katika sekta ya utalii kwa kuimarisha sheria na sera za kulinda haki za mwanamke katika sekta ya utalii.


Aidha Dk Stegomena ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanawake kutendea haki nafasi wanazopewa ili kuondoa dhana ya wanawake kuwa hawawezi na kuwataka wale wote wanaobeza wanawake kuwa hawawezi kuondokana na dhana hiyo potofu.


"Wanawake mkiamiwa mkapewa nafasi zitendeeni haki nafasi hizo ili tuendelee kuaminika kama ambayo Rais Dk,Samia ameonyesha mfano katika kuongoza nchi na kujenga imani kwa mataifa makubwa Duniani".


Alisema katika mkutano huo mada 17 zitajadiliwa katika kongamano hili ikiwemo ukatili wa kijinsia, mchango wa Sekta ya Mali Asili na Utalii katika Maendeleo ya Wanawake na Mafanikio ya azimio la Beojing katika kuimarisha usawa wa Kijinsia hapa nchini".


Kwa upande wake Naibu waziri wa wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Mwanaidi Ally Khamisi alisema amepanua wigo wa kutoabfursa za uongozi kwa wanawake ambapo wanawake asilimia 36 ni mawaziri,wabunge asilimia 37 na mabalozi asilimia 21.




















Comments