ARUSHA BADO YAENDELEA KUNUFAIKA NA MABILIONI YA DKT SAMIA YA KUILETA DUNIA KUKUTANA KWA PAMOJA TANZANIA.
By Lucas Myovela - Arusha.
Viongozi mbalimbali wamempogeza Mhe. Dkt. Samia SuluhuHassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuridhia na kuelekeza fedha kwa ujenzi wa kituo cha Mikutano Cha kimataifa cha Mlima wa Kilimanjaro kitakachojengwa jijini Arusha.
Kituo hicho cha aina yake Afrika, ambacho kinajengwa kwa ubia baina ya Taasisi ya Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa Arusha (AICC ) na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ujenzi wake utakamilika ndani ya miaka miwili.
Pongezi hizo zimetolewa Machi 8, 2025 jijini Arusha wakati wahafla ya utaiji saini hati ya makubaliano ya Ujenzi baina ya wabia PSSSF na AICC.
Akizungumza mbele ya waalikwa waliohudhuria Shughuli hiyo , Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Pindi Chana ambaye wizara yake ni mmoja wa mdau muhimu sana katika matumizi ya Kituo hicho.
Waziri Chana amemshuku na kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasaan, kwa kuelekeza fedha za ujenzi wa kituo hicho huku akiwaomba wasimamizi kuhakikisha kuwa ujenzi unaende haraka ili uweze kutumika kwa mikutano mikubwa ikiwemo ule Mkutano wa Dunia wa masuala ya nyuki na asalia mbao unatarajiwa kufanyika nchini mnamo mwaka 2027.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alimshukuru Mhe. Rais kwa kutoa baraka za ujenzi wa kituo hicho utakao gharimu shilingi 385 bilioni. Pia Waziri Kombo aliishukuru taasisi ya PSSSF kwa utayari wake na kutekeleza maelekezo ya mamlaka.
Akizungumzia Faida nyenginezo, Waziri Kombo alisema uwekezaji huo ni mkakati waSerikali unaolenga kukuza utalii wa mikutano yaani conference tourism.

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajiri wa Hazina, Bi. Neema Musomba alisema, “Msajili wa Hazina anapongeza ushirikiano wa PSSSF na AICC, na kuwa ofisi ya Msajili wa Hazina wakati wowote itakuwa tayari kuhakikisha mradi huu unafanikiwa.”
Nao watendaji wakuu wa PSSSF na AICC kwa nyakati tofauti walisisitiza kutimiza wajibu wao ili kuhakikisha mradi huokimkakati unakamilika kama ilivyopangwa.
Comments
Post a Comment