DKT. BITEKO AWAAGIZA TANESCO KUPELEKA NGUZO 25 MUNDARARA, AWAPONGEZA WACHIMBAJI WA VITO KWA MAENDELEO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA MADINI. FEMATA WATOA TAMKO, BILIONEA SENDEU AKABIDHI MADAWATI 300.

🔻FEMATA WAIUNGA MKONO SERIKALI YA DKT SAMIA WAAPA KUMPA KURA ZAIDI YA MILIONI 6.


🔻AMUAGIZA MENEJA WA TANESCO KUPELEKA NGUZO 25 ZA UMEME NA KUHAKIKISHA UMEME WANAWAKA KATIKA VIJIJI VYA MUNDARARA.

Na Lucas Myovela - Longido Arusha.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amewapongeza wachimbaji wa madini ya vito katika machimbo ya Mundarara yaliyopo wilayani Longido Mkoani Arusha kwa kuendelea kuikuza sekta hiyo kwa maslahi mapana ya Taifa na ukuaji wa uchumi.
Dkt. Biteko ameyasema yayo leo April 24, 2025 katika mkutano wa hadhara uliyofanyila katika kata ya mundarara wilayani Longido katika ziara yake kuelekea kilele cha siku ya Muungano wa Tanzania.


Dkt. Biteko ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha inatatua changamoto zote za wananchi wa kata ya Mundarara zinazo wakabili ikiwemo zahanati, barabara pamoja na umeme.


"Nimewasikiliza kuwa umeme mliyo nao bado kuna changamoto ya barabara na kuna upungufu wa nguzo za umeme 25 kufikia vijiji vingine ili kufanya kazi usiku na mchana niwakikishie nguzo hizo zinawekwa kuanzia sasa ili shughuli za uzalishaji ziendelee kwa kasi na kwa ujenzi wa Taifa letu". Amesema Biteko.


"Namuagiza Meneja wa Tanesco kuhakikisha nguzo hizo zinafika haraka na wanachi wanapata umeme kwaajili ya kuendelea kufanya kazi usiku na mchana". Amesema Dkt. Biteko.

Pia Dkt. Biteko amewaomba wananchi kuulinda Muungano wa Tanzania, utaifa, utamaduni na amani ya taifa kuelekea kipindi cha uchaguzi na kuwataka wanachi kuweza kuwasikiliza kila mmoja anae wafata na kuwachagua viongozi wanao wataka na wanaofanya kazi.


"Nyie wana Mundarara mnajuia ilivyo kuwa kipindi cha nyuma msikubali mti awagawanye kwa ajili ya vyeo na madaraka ili haya mnayo endelea kuyafanya katika uwekezaji yaweze kuza matunda kwa maslahi mapana ya taifa". Amesisitiza Dkt. Biteko.

Kwa uande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya R-GI CO LTD ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya vito FEMATA Ndg. Prosper Tesha, Ameishukuru serikali kwa kuwapatia umeme migodini kitu ambacho kimeleta mabadiliko makubwa na ya uhakika katika sekta ya madini.


Aidha ameeleza kuwa katika awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya madini imeweza kuchangia pato la Taifa kwa 10.1% hadi kufika mwaka wa fedha 2024 /2025 kitu ambacho kimetokana na sera, na usimamizi mzuri wa Wizara ya madini chini ya Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde na wasaidizi wake.

Aidha mwenyekiti huyo ameeleza kuwa hadi sasa wachimbaji wote wa madini ya vito nchini ni zaidi ya milioni sita na watanzania wengi bado wanahamasika kuingia katika sekta ya madini kuendelea kunufaika na rasilimali za Taifa la Tanzania.


"Tumekubalia na Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wa madini nchini Ndg. Johm Wambura Bina na wanachimbaji wote tulidhia kuunga mkono serikali ya awamu ya sita kubaki madarakani na kupiga kura za ndiyo za kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kishondo kwa kura zote ambazo ni zaidi ya milioni sita.


Aidha ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan wamejivunia na kuona mabadiliko makubwa katika Sekta ya Madini pamoja na sekta nyingine zinazo husu jamii na kufanya taifa kuwa lenye mafanikio makubwa kiuchumi.

Aidha kwa upande wake Muwekezaji na mchimbaji wa madini hayo adhimu ya ruby Ndg. Sendeu Layzer amekabidhi madawati 300 katika shule za kata ya mundarara ambapo ameeleza kuwa huo ni muendelezo wa kurudisha kwa jamii kutokana na faida alizopata katika uchimbaji huo wa madini ameweza kurudisha kwa wananchi zaidi ya milioni 500.


"Naishukuru serikali baada ya kupata madini na kutangazwa kuwa bilionea, Serikali iliweza kunishauri namna bora ya kuendeleza mtaji huu na mafanikio nimeyaona hadi leo kampuni yangu tunaendelea kuchangia kwa jamii na leo hii naikabidhi serikali madawati 300". Amesema Sendeu.




Comments