#BREAKING: PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA.

  KWAKHER PAPA FRANCIS KANISA KATOLIKI DUNIA LINAKULILIA.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amefariki dunia leo April 21,2025 Jumatatu ya Pasaka katika makazi yake ya Casa Santa Marta.

Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 ambapo Vatican imethibitisha na kusema Papa amefia kwenye makazi yake Vatican na taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitatolewa.


Papa ambaye alizaliwa mwaka 1936 hivi karibuni amepitia changamoto ya upumuaji hadi kuhitaji mashine ya kusaidia kupumua na amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu(nimonia) hadi kupelekea kulazwa kwa wiki kadhaa kabla ya baadaye afya yake kuimalika.


Papa Francis, ambaye alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki mwaka 2013, alikuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini na mmoja wa mapapa wa umri mkubwa zaidi kuwahi kuliongoza Kanisa hilo.


HABARI KAMILI.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis alifariki dunia Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican.


Muda mfupi uliopita, Mwadhama, Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, kwa maneno haya:

"Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko''.


Saa 7:35 asubuhi ya leo (saa za huko), Askofu wa Roma, Francis, alirudi nyumbani kwa Baba. Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa Lake."


"Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa ajili ya maskini zaidi na waliotengwa zaidi."


Farrell anaongeza: "Kwa shukrani nyingi sana kwa ajili ya kielelezo chake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaipongeza roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu Mmoja na wa Utatu."


Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter's Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka.


Alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter's kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: "Ndugu wapendwa, Pasaka njema."


Hotuba yake ya Pasaka na baraka ilisomwa na msaidizi alipokuwa ameketi, akitazama.


Baada ya baraka, alizungushwa kwenye uwanja. Alipopita katikati ya umati, msafara wake ulisimama mara kadhaa huku watoto wachanga wakiletwa ili awabariki.

Comments