RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA MADARAJA MAWILI MUHIMU YANAYO UNGANISHA MIKOA YA KASKAZINI. UJENZI KUKAMILIKA JULAI 2, 2025.

RC MAKONDA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA MADARAJA YA KING’ORI BARABARA YA ARUSHA – MOSHI.

Na Lucas Myovela -Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, leo asubuhi amefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa madaraja mawili ya King’ori yanayojengwa katika barabara kuu ya Arusha – Moshi na kuridhishwa na kasi na ubora wa ujenzi wa madaraja hayo ambayo ni kiunganishi muhimu kati ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Makonda amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuboresha miundombinu ya usafiri nchini, hasa maeneo ambayo yamekuwa na changamoto kubwa wakati wa mvua ambapo serikali imechukua hatua hiyo baada ya wananchi kadhaa kupoteza maisha katika eneo hilo mwaka uliopita kutokana na changamoto za miundombinu hafifu.

"Serikali ina wajibu wa kulinda maisha ya wananchi wake, ndiyo maana tumetafuta suluhu ya kudumu kwa kujenga daraja imara badala ya makalvati yaliyokuwa yakisababisha madhara na hii ni hatua kubwa ya maendeleo katika kuhakikisha usalama wa barabara hii muhimu.” Amesema Mhe. Makonda.


Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhakikisha miundombinu ya barabara nchini inaboreshwa na kuwa salama wakati wote – iwe ni kipindi cha mvua au kiangazi pamoja na kuipongeza Wizara ya Ujenzi na taasisi husika kwa kutekeleza kwa ufanisi maelekezo ya Mhe. Rais.


Hata hivyo, mesisitiza umuhimu wa watumiaji wa barabara kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili miundombinu hii iweze kudumu kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kuwa barabara hii inapita magari makubwa ya mizigo na pia hutumiwa na watalii wengi wanaotembelea maeneo ya kitalii ya Kaskazini mwa Tanzania.

“Natoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhepp Rais. Badala ya maneno, tuongeze bidii ya kufanya kazi na kutafuta fedha halali. Hii ndiyo njia ya kweli ya kuleta maendeleo ya kweli kwa taifa letu,” ameongeza.


Mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 4.6 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2, 2025.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Eng. Martin Bouchard kamala kutoka kampuni ya Abemulo contractors co Ltd wanaotekeleza mradi huo ameeleza kuwa mpaka sasa mradi unaendelea salama mbali na changamoto za mvua kuendelea kunyesha wanajitahidi kwa kila hali ili kumaliza mrasi huo ndani ya wakati.

"Mvua zisipo kuwa kubwa ni imani yangu mradi huu tutamaliza mdani ya mkataba ila kama mvua zitazidi itabidi tufanye kadri tuwezavyo na itabidi tuombe ongezeko la muda ili kufanya kazi kwa ufanisi na ubora wenyeviwango vikubwa". Amesma Eng. Kamala.












Comments