🔻AWAONYA VIKALI WAHARIBIFU WA BARABARA ARUSHA, ATOA KONGOLE KWA TANROAD.
🔻RC MAKONDA ATOA RAI KWA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA.
Mhe. Makonda ametoa rai hiyo leo 20 Mei, 2025 wakati akikagua upandaji miti kwenye barabara ya Moshi - Arusha zoezi alilozindua mwenyewe mapema mwezi Februari mwaka huu ambapo amesema Suala la Utunzaji wa mazingira sio jukumu la Serikali peke yake bali ni la kila mwananchi.
Amesema kwa kufanya hivyo Mkoa wa Arusha utakuwa na hali ya hewa nzuri na mazingira ya kuvutia nyakati zote za masika na kiangazi.
“Hatutaki Arusha iwe ni ya watu wasio wastaarabu, kwasababu uwezo wa kuwa wasafi tunao na uwezo wa kuwa na mazingira bora tunao.” Amesema Mhe. Makonda.
Katika hatua nyingine amewapongeza Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kwa kuendelea kusimamia upandaji wa miti kwenye njia hiyo sambamba na kuweka kingo kwenye maeneo hayo ili kuzuia wananchi kukatiza katikati ya barabara ambapo miti imepandwa.
Comments
Post a Comment