BILIONI 10 KUIBADILISHA ARUSHA KIUCHUMI:

🔻RC MAKONDA ATAKA MIKATABA ISAINIWE HADHARANI WANANCHI WAWEZE KOHOJI ISIPO KAMILIKA KWA WAKATI.

Na Lucas Myovela - ARUSHA.Halmashauri ya Jiji la Arusha meweka historia nyingine kuwa kwa kufanya Makubaliano na kutiliana saini mikataba miwili ya ujenzi wa uwanja wa mpira pamoja na ujenzi wa soko la machinga. Miradi hiyo inayotekelezwa inayo jumla ya shilingi Bilioni 10,324,288,119.57. Ambapo ilupatikanaji wake umefanyika kupitia njia ya manunuzi umma (NeST) kwa njia ya ushindani na kupata wakandarasi wawili watakao tekeleza miradi hiyo.

Mradi wa kwanza wenye gharama kubwa ni ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unatekelezwa na Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya STC Construction co Ltd alitunukiwa tuzo ya zabuni kwa gharama ya shilingi bilioni 9,614,158,878,60. Pamoja na kodi ya ongezeko la thamani ya msimamizi mshauri.

Mradi wa pili ni ujenzi wa soko la machinga ambapo mkandarasi ni kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT Construction Company LTD ambapo anatekeleza mradi huo kwa Gharama ya shilingi milioni 710,129,240.97. Pamoja na kodi ya ongezeko la thamani.


Makubaliano hayo yamefanyika juni 17,2025, katka vanja vya utekelezaji wa mradi wa soko la machinga na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda pamoja na wananchi kwa wakandarasi wa kampuni hizo na kushudiwa na wananchi,viongozi wadini,siasa,wanamichezo akiwemo Rais wa TFF.

Akiongea mara baada ya kusaini kandarasi hiyo Meneja wa Suma JKT Ujenzi kanda ya Kaskazini, Luteni Kanali mhandisi Daud Zengo alisema kampuni yake inatekeleza mradi wa ujenzi wa soko hilo la machinga na wanatarajia kukamilisha ndani ya muda uliopangwa wa miezi sita kama walivyokubaliana ili kupisha shughuli za uzalishaji ziweze kuendelea.

"Leo tumesaini kandarasi kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa soko la machinga baada ya kampuni yetu kushinda zabuni ambapo mkataba wetu ni miezi sita na tunatarajia kumaliza kazi hii kwa wakati na ikiwezekana tutamaliza kabla ya muda wa makubaliano. tutafanyakazi kwa uadilifu kwa kuzingatia ubora unaotakiwa kwa kazi tunazopewa na serikali ili kujenga uaminifu kwa kampuni yetu hii ya kizalendo iliyopo chini ya serikali". Amesema Luteni Kanali Zengo.

Awali Dkt. Maduhu Nindwa kisoma taarifa fupi ya miradi hiyo miwili kwa niaba ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,John Kayombo. Dkt.Nindwa ameeleza kuwa miradi hiyo ni sehemu ya chanzo cha mapato ya halmashauri ya Jiji la Arusha na itaongeza wigo wa kukusanya mapato ya halmashauri hiyo na kuchochea uchumi wa taifa.


"Lengo la ujenzi wa uwanja huu wa michezo ni chanzo cha mapato kwa jiji la Arusha pia ni maandalizi ya mashindano ya michuano ya Afrika (AFCON) na kusaidia kukuza vipaji vya michezo mbalimbali katika jiji letu Arusha". Amesema Dkt. Nindwa.


"Uwanja huu utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 8000 kwa pamoja,Utakuwa na viwanja 3 vya michezo ya pete,kikapu pamoja na tenesi,Utakuwa na ofisi nane, Vyumba vya kubadilishia nguo vinne,Kumbi ya watu mashuhuri VIP, Fremu za maduka 98,Matundu 50 ya vyoo, Mageti 12, Eneo la maegesho magari 150 magari ya kawaida 133 na magari ya VIP 12 pamoja na mabasi matano". Ameongeza Dkt. Nindwa.

"Lengo la mradi wa Soko la machinga ni kutoa huduma kwa jamii,kuongeza wigo na ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuwezesha wafanya Biashara ndogondogo kufanya kazi zao katika mazingira mazuri, Soko hili likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukuwa wafanyabiashara ndogondogo zaidi 80, kutakuwa na huduma ya vyoo na sehemu ya huduma ya chakula". Alieleza Dkt. Nindwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alijivunia kuona utekelezaji wa miradi hiyo iliyokuwa imesimama kwa muda mrefu ikisainiwa,licha ya kuwepo kwa mipango hiyo na fedha kutengwa tangu mwaka 2021.


Makonda alisisitiza kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jiji la Arusha sio mipya bali ilikuwepo, akitolea mfano ujenzi wa soko la wamachinga alisema fedha zilitolewa na rais Samia Suluhu hasani kiasi cha sh,milioni 500 tangu mwaka 2021 lakini fedha zilikaa kwenye akaunti ya halmashauri ya jiji la Arusha bila kufanya kazi iliyokusudiwa kwa sababu ya mvutano wa viongozi.

"Nilipofika Arusha niligundua kuna fedha zimetolewa na rais Samia kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Machinga nilipowauliza kwa nini hawajengi hilo soko wakati fedha zipo,walisema kila wanapokaa na viongozi wa machinga na kukubaliana anaibuka mtu na kwenda kuwashawishi machinga wasikubali kujengewa soko eneo hilo". Alisema Makonda.


"Niliwaambia viongozi wa Jiji la Arusha, huu mwaka ukiisha soko halijajengwa, basi ama zao ama zangu. Leo nimefika hapa kushuhudia hatua hii muhimu mbele ya wananchi na tunataka miradi yote yenye fedha tayari itekelezwe kabla ya mwezi Julai ili wananchi waanze kunufaika".Aliongeza Makonda.

Alisema tangu ameingia Arusha amefanikisha kusukuma miradi mbalimbali iliyokuwa imekwana ukiwemo mradi wa ujenzi wa Stendi ya mabasi eneo la Bon city ,Soko La Kilombero, Ukumbi wa Mikutano,Uwanja wa Michezo,Uwanja wa Mpira wa Afcon na ujenzi wa barabara za Lami ambayo kwa sasa anaona fahari miradi hiyo inatekelezwa kwa kasi kubwa na aliahidi hadi ifikapo julai 1mwaka huu hakutakuwa na mradi wowote ambao hautekelezwi.


Katika hatua nyingine Makonda amegawa pikipiki 23 pamoja na Bajaj mbili kwa watendaji wa kata zote za jiji la Arusha kwa ajili ya kuwarahisishia shughuli zao za kiutendaji kuwatumikia wananchi.


Makonda akifafanua kwamba fedha za kununua vyombo hivyo vya moto ni sehemu ya sh,milioni 300 zilizotengwa na halmashauri ya jiji hilo kwa ajili ya kununua gari la mstahiki meya .


"Nilimwomba mstahiki meya tubadilishe matumizi ya fedha hizo badala ya kununua gari la kifahari nilimshauri tununue vitendea kazi vya watendaji na fedha zilizobaki takribani milioni 180 nimeelekeza zijenge vivuko vya madaraja"Alisema.

Naye meya wa jiji la Arusha Maxmilian Iranghe alisema kuwa katika kipindi cha Miezi sita halmashauri ya jiji la Arusha imeweza kusaini miradi ya zaidi ya bilioni 60 iliyotokana na jitihada kubwa za mkuu wa mkoa Makonda.


"Katika kipindi cha Miezi sita jiji la Arusha limefanikiwa kununua mitambo ya kutengeneza barabara,Mradi wa ujenzi wa stendi ya Bondeni city ,soko la kwa morombo ,Soko la Kilombero na eneo la mapumziko bustani ya Mto Themi"Alisema Meya.



















Comments