MCHENGERWA AAGIZA MADIWANI WOTE NCHINI WANAO MALIZA MUDA WAO KUTORUDISHA VISHIKWAMBI.

🔻AMTAKA KATIBU MKUU TAMISEMI KUSIMAMIA HILO, AMPONGEZA RC MAKONDA KUINYANYUA ARUSHA KIMAENDELEO.

🔻MAKONDA AAGIZA WENYEVITI WOTE KUANZIA NGAZI ZA VITONGOJI KUWEKEWA POSHO ZAO KWENYE AKAUNTI ZAO NA SIO KUZIFATA KWA WATENDAJI.Na Lucas Myovela - Arusha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemwangiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Adolf Ndunguru kuwaandikia wakurugenzi wa Halmashauri kutokuchukua vishikwambi walivyokuwa wanatumia madiwani waliomaliza muda wao pamoja na stahiki zao.


Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo mapema leo Juni 20, 2025 ambayo ni siku ya mwisho ya mabalaza yote ya madiwani kuvunjwa kote nchini ili kupisha michqkato ya uchaguzi wa Mkuu mwezi Oktinba 2025.


 Mchengerwa ameeleza hayo baada ya kupigiwa simu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda wakati akiongea na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kikao cha kuvunja balaza hilo ambalo limedumu kwa miaka 5.


Waziri Mchengerwa amesema kuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia yametekelezwa vyema kupitia usimamizi madhubuti wa Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

"Ni kazi ya nguvu, jasho, ubunifu na stadi za madiwani kote nchini. Nawapongeza Mameya wote kwa kazi yao kubwa, hususan Meya wa Jiji la Arusha. Kazi yao imeandikwa katika kitabu cha dhahabu kwa kuwa wamewahudumia wananchi wanyonge kwa moyo wa uzalendo," amesema Mhe. Mchengerwa.


Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Makonda, kwa kazi kubwa na yenye mafanikio anayoifanya mkoani humo, akisema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI inatambua na kuthamini jitihada zake.


"Nichukue nafasi hii kuongea na taifa kupitia baraza hili la madiwani wa Arusha kumuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha madiwani wote kote nchini hawarudishi vishikwambi walivyo kuwa wanavitumia ili hii ibaki kuwa ni alama nzuri kwao kwa jinsi walivyo litumikia taifa hasa katika awamu ya kwanza katika serikali ya Awamu ya 6 inayo ongizwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan". Amesema Mchengerwa.


"Najua kwasasa tunaelekea katika uchaguzi Mkuu na tunakila sababu ya kuhakikisha Dkt. Samia Suluhu Hassan anamalizia ungwe yake ya pili katika awamu yake ya sita ya kuliongoza taifa letu la Tanzania niwahakikishie hata stahiki zenu mtazipata kwa wakati ili na nyinyi mkafanye mipango yenu mliyo jipanga nayo". Ameongeza mchengerwa.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda, Awaagiza wakurugenzi wa halamshauri zote za Mkoa wa Arusha kuwalipa madiwani stahiki zao zote yakiwemo mafao yao kwa wakati kwa sababu ni takwa la kisheria na kama kuna changamoto yeyote wawasiliane na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha.

"Pia nawaagiza wakurugenzi wote Mkoa wa Arusha kuhakikisha posho za wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji ziingizwe kwenye akaunti zao za benki moja kwa moja tofauti na hivi sasa ambapo zinatumwa ofisi za watendaji wa Kata kitu ambacho kinaondoa hamu ya utendaji kazi lazima tuwajali na kuwathamini siyk kuwakumbuka wakati wa matukio tu". Amesema Makonda.


"Hii ni pamoja na kuwapelekea nakala za miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao yote katika bajeti ya kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka huu wa 2025-2026 ili waifahamu vizuri na kila mtendaji wa serikali akitaka kutekeleza mradi katika maeneo yao lazima viongozi hao wapate taarifa". Ameongeza Makonda.


Aidha Makonda ameeleza kuwa kwasasa mikakati mikubwa ni kuifanya Arusha kuwa Jiji la Kioekee katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati na kuwataka watanzania wenye maeneo makubwa kuchangamkia gursa za uwekezaji ikiwa ule wa ujenzi wa bandari kavu pamoja na maeneo ya uwekezaji mengine ili kuzidi kuupanua Mkoa wa Arusha.




Comments