VUNJO KUNACHANGAMKA TESHA ACHUKUA FOMU KUWATUMIKIA WANA VUNJO AOMBA CHAMA CHAKE KIMPE RIDHAA.

VUNJO KUNACHANGAMKA TESHA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE KUWATUMIKIA WANA VUNJO.

Na Lucas Myovela - Kilimanjaro.

Sasa ni Rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya R-GI na Mwenyekiti wa Madini ya Vito Taifa (FEMATA), Daudi Prosper Tesha amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la VUNJO Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 2025 endapo atapewa ridhaa na chama chake.


Tesha amechukua fomu hiyo katika ofisi za Chama Wilayani Vunjo Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wake kikatiba kama mwanachama hai wa CCM ambaye yupo tayari kwaajili ya safari ya mafanikio ya kulijenga taifa na kuinua uchumi kwa wananchi wa Vunjo.


Tesha ambaye amejipambanua kwa kueleza kuwa kwasasa taifa linakuwa kwa kasi katika sekta mbalimbali kutokana na juhudi zinazo fanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan, na yeye kama mwanachama wa CCM yupo tayari kuwatumikia wananchi wa Vunjo ili kuleta mafanikio na kurejesha matumaini mapya kwa watanzania wa Jimbo lake.


"Kwasasa taifa linahitaji damu changa kwaajili ya mapambano ya kiuchumi na sisi kama vijana tmepewa fursa na chama chetu hatupaswi kubaki nyuma lazima tutoke tuunganishe nguvu kwa pamoja kwa ujenzi wa taifa letu la Tanzania yapo mengi ya kusema ila kwasasa siyo wakati wake kwasasa nimetekeleza haki yangu ya kikatiba". Ameeleza Tesha.


Aidha kwasasa uchukuaji wa fomu kwa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) unaendelea nchi nzima katika makundi yote ya kuwania nafasi za ungozi katika vyombo vya dola hapa nchini na zoezi hilo limepangwa kutamatika Julai 2, 2025.



Comments