CHIKU ISSA MGOMBEA UBUNGE ARUSHA VITI MAALAMU NA WENGINE NANE.

NYOTA YAANZA KUWAKA SASA KUTINGA BUNGENI BAADA YA UCHAGUZI WA OKTOBA 2025.

Leo Julai 29, 2025 Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM ) CPA, Amoss Makala ametangaza rasmi majina ya wanachama wa chama hicho waliyopitishwa na kamati kuu ili kuwania nafasi za ubunge katika majimbo yote Tanzania bara, Zanzibar pamoja na majina ya wabunge wa viti maalum na makundi maalum.


Akisoma majina ya wagombea wa viti maalum upande wa Tanzania Bara amesema kuwa Chama kimetua majina 8 kwa Mkoa wa Arusha ya wagombea nafasi za Ubunge wa Viti Maalum ambapo Miongoni mwao ni Chiku Athuman Issa na wengine.


Chiku Athuman Issa ambaye ni kada mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi na mwenyemaono ya kimaendeleo katika kulijenga taifa na mtu ambaye amehudumu katika nafasi mbalimbali uongozi.  


Aidha Chiku amewahi kuhudumu katika taasisi ya fedha ya benki ya CRDB kama Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa benki hiyo kubwa hapa nchini na kufanikisha hatua mbalimbali za kimabadiliko na maendeleo katika sekta ya kifedha.


Pia Chiku Athumani Issa ni Mjumbe wa kamati ya Uchumi, Mpango na Fedha UWT Taifa, Mjumbe wa Mkutano UWT Taifa na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji wilaya Arusha jiji.


Kufuatia kwa Chama cha Mapinduzi (CCM ) kuweka wazi majina ya wanachama wao tayari ni kiashiria cha moshi mweupe wa wagimbea hao kwenda mbele ya wajumbe na kuomba lidhaa ya kuchaguliwa ili kuweza kupata fursa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2025.


Comments