MWAMBA LUKUMAY SASA TAYARI KUSUBILI KIPYENGA NDANI YA CHAMA.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Rasmi leo Elias Lukumay amerejesha fomu yake ya ubunge na kutimiza jukumu lake la kikatiba ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) ma kusubili mchakoto ndani ya chama kurudisha majina matatu ya wagombea ambao watapigiwa kura na wajumbe wa jimbo husika na kisha kupata jina la mtu mmoja ambaye atapeperusha bendera katika uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 2025.
Joto la uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Magharibi Mkoani Arusha linazidi kupanda kiasi na kuibua mtikisiko baada ya Kada Maarufu wa Chama cha mapinduzi Ndg. ELIAS LUKUMAY Kuchukua Fomu ya ubunge June 29.2025 ili kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo pale atakapo pewa ridhaa na chama chake.
Lukumay ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa Malori TANZANIA (TATOA)hatimaye amejitosa rasmi katika duru hizo baada ya kuwepo uvumi wa muda mrefu kuhusu kugombea katika jimbo hilo.
Kuchukua fomu kwa Elias Lukumay kunaongeza joto la uchaguzi kwa wanasiasa wa chama cha mapiduzi katika jimbo la Arumeru magharibi ambapo hadi sasa kila mmoja anasubilia kurejeshwa kwa jina lake kupitia chama cha mapindizi ambapo alichukua fomu June 29. 2025.
Comments
Post a Comment