KAYOMBO KUVIPIGA TAFU VILABU VYA MPIRA NA VYAMA VYA KIMICHEZO ARUSHA.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha John Kayombo, amevitaka Vilabu vya mpira na vyama vya michezo kuwasilisha mipango kazi yao ili waweze kusaidika na kukuza tasnia ya michozo hapa nchini.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga bonanza la michezo la Sabasaba ambalo limefanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa iliyopo kata ya Moshono Jijini Arusha ambalo limeandaliwa na timu ya Mwangaza Veterans.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Afisa utamaduni na michezo jiji la Arusha Benson Maneno, Ameeleza kuwa hadi sasa serikali imewekaza miundombinu ya kutosha katika sekta ya michezo hizo mi fursa kwa vijana wa Mkoa wa Arusha kutendea haki vipaji vyao kama sehemu ya ajira.
"Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha imejipanga kuweza kuzisaidia timu na vyama vya kimichezo ambavyo vitakuwa tayari kupeleka mipango kazi yao kwa ajili ya faida ya michezo katika jiji letu la Arusha". Amesema Maneno.
Amesema wamejipanga kuhakikisha Arusha inapiga hatua katika michezo ikiwemo kuwa na timu ya Ligi Kuu na kuifanya kurejesha heshima yake kama zamani ilipokuwa na timu za AFC,977KJ FC,Palsons FC ambapo kwa kuanza wameanza na ujenzi wa uwanja wa Soka ambayo inajengwa New Arusha City.
“Tuko tayari kushirikiana na mdau yeyote ambaye yuko kuwekeza katika michezo na niwaombe Klabu na vyama leteni mipango kazi yenu ofisi yangu itakuwa tayari kutoa ushirikiano”.Amesema Maneno.
Katika hatua nyingine jiji la Arusha imeweka wazi kuwa itashirikiana na timu ya Mwangaza Veterans kuboresha uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa ili kutoa nafasi ya vijana na wazee kushuudia burudani.
Uwanja huo utafanyiwa maboresho kataika sehemu ya kuchezea (pitch) lakini pia uwekaji wa taa ambayo itatoa nafasi ya michezo kufanyika usiku ,pia itaifanya Baraa kuwa shule ya kwanza jijini Arusha kuwa na uwanja wenye taa.
Haruni Kidungu ni katibu wa Mwangaza Veterans alisema kama mpango wao wa kufanyia maboresho uwanja wa Baraa utafanikiwa basi itatoa fursa kwa wadau wa michezo Arusha kuweza kushuudia burudani ya soka kutoka kwa vijana na wachezaji wa zamani (veterans) ambao wanatumia uwanja huo.
"Tunatarajia kuwasiliana na ofisi ya mkurugenzi wa jiji kuboresha uwanja huu wa Baraa na bahati nzuri afisa michezo amekuwepo leo na kututaka twende jumanne naamini ombi letu litafanikiwa na tutaiboresha kwa ajili ya faiida ya visazizi vijavyo".Amesema Kidungu.
Akizungumzia bonanza la Sabasaba ambayo imeshirikisha timu sita za Mwangaza, AICC Kijenge,KMKM ya Zanzibar,Free Stress ya Dar na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela.
Alisema ushindani ulikuwa mkubwa ,ni msimu wa sita wa muchuano hiyo lengo ni kuwaweka pamoja wachezaji wa zamani hada katika kudumisha umoja na mshikamano pia kwa ajili ya kuboresha afya.
Naye Fredrick Lyimo “Deco” ,ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Wilaya ya Arusha Mjini (ADFA),ameipongeza Mwangaza Veterans kwa kwa kuandaa bonanza ambalo limelenga kuwaweka pamoja wachezaji wa zamani lakini pia kurudisha kwa jamii kile ambacho wanakipata.
“Kama uongozi tuko tayari kutoa ushirikiano muda wowote kwa timu zote hapa Arusha lengo letu ni lazima soka hapa Arusha lichezwe”.
Sabasaba bonanza mwaka huu 2025 imekuwa ni timu ya AICC Kijenge kutoka Arusha,mshindi wa pili KMKM Zanzibar na mshindi wa tatu Mwangaza Veterans Arusha.
Comments
Post a Comment