WAVUKA LENGO 2024/2025, WAREJESHA KWA WALIPA KODI TRILIONI 1.2 HAIJAWAHI KUTOKEA.
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 08, 2025) alipofungua kikao kazi cha Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha Mikutano cha Arusha (IACC).
“Nendeni mkachunguze hawa wanaokuja kufanya biashara nchini, kama wanaondoka na mapato yetu kwa kutolipa kodi yetu, ni lazima tubane eneo hilo kama ambavyo sisi tunabanwa tunapokwenda kwao, yeyote aliyeamua kuja kufanya biashara Tanzania ni lazima ajue Tanzania ina sheria zake ikiwemo za ulipaji kodi”. Mesema Majaliwa.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza TRA kwa kufanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 32.26, sawa na ufanisi wa asilimia 103.9 dhidi ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 31.05.

Katika hatua nyingine, Mhe. Majaliwa ameiagiza Wizara ya Fedha kuendelea kufanya maboresho ya Sera, sheria na kuimarisha mifumo ya kodi ili kufikia wigo wa juu wa ukusanyaji kodi bila kuathiri ustawi wa shughuli za kiuchumi.
“Kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ubunifu mliouonesha mkapata mapato makubwa, endeleeni nao, ubunifu huu umeleta mafanikio makubwa, mbinu rafiki na zakitaalamu mnazotumia kukusanya kodi ziendelezwe, sambamba na kuzingatia Sheria, Utawala Bora, Kanuni na utu”. Amesisitiza Majaliwa.

“Wengi wanadhani kuwa fedha za maendeleo zipo Benki Kuu, tunatakiwa kuendelea kuwaelimisha Watanzania kwamba kila kitu cha maendeleo wanachokiona ni fedha zetu, hata fedha za mkopo ni fedha zetu kwa kuwa tutalipa kwa kodi zetu”. Ameeleza Dk. Nchemba.

“Na katika mwaka huu wa fedha tumepanga kukusanya shilingi trilioni 36 ikiwa ni mapato ghafi, tunaamini tukiwa pamoja na walipa kodi tunafanikiwa, tunajua hii ni ndoto ambayo viongozi wetu mnatamani tuitimize”. Ameeleza Mwenda.
Comments
Post a Comment