MARTHA GIDO NA CHIKU ISSA WAWANG'OA VIGOGO UWT ARUSHA.

CATHELINE MAGIGE NA ZAITUNI SWAI WAANGUKIA USO KWENYE ZEGE ZITO LA WAJUMBE.

Na Lucas Myovela - Arusha.

MUHTASARI: Wagombea wapya wa nafasi ya ubunge wa viti maalum Mkoa wa Arusha wameng'ara katika uchaguzi huo uliyo fanyika hapo jana Julai 30, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC.

Kufuatia Mchakato wa upigaji kura kwa wagombea nane wa nafasi ya ubunge wa viti maalam Mkoa wa Arusha waliyoteuliwa na kamati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutangazwa na Katibu wa itkadi na uenezi wa chama hicho CPA, Amoss Makala, Julai 29, 2025 umekuwa wa kukata na shoka baada wabunge waliyokwa wakitetea nafasi zao kupigwa chini na wajumbe.


Majina mapya ya wagombea wa nafasi hiyo yameonekana kushika kasi kwa wajumbe hao kitu ambacho kimebadilisha upepo na kuwaacha midomo wazi wabunge waliyo kuwa wanatetea nafasi zao za ubunge.


Majina ya Chiku Issa na Martha Kivunge yalionekana kutoa moshi mweupe dakika za mwanzo wa uhesabuji wa kura baada ya kupigwa na wajube wapatao 1261 katika Mkoa huo wa Arusha.


Uchaguzi huo ulifanyika na kusimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Laban Kihongosi na kuhudhuliwa na viongizi mbalimbali wa chama pamoja na wajumbe husika.

Mtanange huo uliwakutanisha wagombea nane ambao ni Lilian Joseph BADI, Zaytun Seif SWAI, Chiku Athuman ISSA, Martha Gido KIVUNGE, Dkt. Asanterabi Ngoyai LOWASSA, Navoi MOLLEL, Martha Martin AMO, Catheline Valentine MAGIGE.


Akisoma matokeo hayo mara baada ya wajumbe kupiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi alisema kuwa wajumbe waliyo hudhudhilia Mkutano huo ni 1261 na wote walipaga kura.


"Idadi ya Kura zilizo pigwa ni 1252, Akidi ya wapiga kura 1661, Idadi ya kura zilizo haribika ni 7, Idadi ya kura halali ni 1245". Alisema Kihongosi.


Akitangaza matokeo hayo Kihogosi alisema kuwa Lilian Joseph Badi amepata kura 9, Martha Martin Amo amepata kura 50, Navoi Mollel amepata kura 95, Zaytun Seif Swai amepata kura 141, Dkt. Asanterabi Ngoyai Lowassa amepata kura 196, Catheline Valentine Magige amepata kura 213, Chiku Athuman Issa amepata kura 775 na Martha Gido Kivunge amepata kura 1004.

Kwa mujibu wa matokea hayo Martha Gido Kivunge ndiyo ameongoza kwa ushindi kwa kupata kura 1004 na Chiku Athuman Issa kushika nafasi ya pili kwa kuoata kura 775 kitu ambacho wajumbe walishangilia na kusema wamepata wabunge wapya watakao itetea na kuilea UWT Mkoa wa Arusha.


USHINDI WA CHIKU NA MARTHA.

Ushindi wa Chiku Issa na Martha Gido unatajwa kuwa chachu ya mabadiliko ya umoja wa wanawake Mkoa wa Arusha ndani ya Chama cha Mapinduzi kutokana na CV zao kuwa bora katika uongozi pindi wanapo pata nafasi.

Chiku Issa ni moja ya watumishi makini waliyojikita katika maswala ya utawala wa fedha, uchumi na siasa kitu ambacho kwasasa kinaonekana kuzaa matunda katika taia la Tanzania.


Chiku Athuman Issa ametumikia taasisi ya fedha ya Benki ya CRDB kama meneja wa kanda ya kaskazini na kwasasa ni Mjumbe wa kamati ya Uchumi, Mpango, Fedha UWT Taifa, Mjumbe wa Mkutano UWT Taifa, Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji wilaya Arusha jiji.


Hadi sasa matamanio ya wanachama wa chama cha mapinduzi ni majina haya mapya yaweze kurudi ili waweze kuwatumikia wana UWT Mkoa wa Arusha.


Kufuatia kanuni za chama mara baada wajumbe kupiga kura majina hayo huchujwa (mchujo wa ndani) ambao utakaoamua nani kati ya wale waliochaguliwa ndio atateuliwa rasmi kufuatia uwiano wa viti maalum wa chama na hupangwakulingana na uwiano wa kura zilizopatikana na chama katika uchaguzi mkuu.


ANGUKO LA CATHELINE MAGIGE NA ZAYTUNI SWAI.

Inaelezwa kuwa kwa kipindi kirefu wawili hao walikuwa na magenge ya kiasiasa kitu ambacho kiliwachanya wanachama na kutofurahia mwenendo wa siasa zao kwa maslahi mapana ya chama.


Bado hadi sasa inatajwa kuwa kila mmoja alifanya vizuri kwa upande wake kwa UWT na kujiimarisha ili asije piteza nafasi yake ila wajumbe wamefika ukomo wa migorogoro ndani ya chama na kutaka kuijenga CCM moja iliyo imara, madhubuti na yenye kutatua changamoto za wananchi.


Je, unahisi ni haya tu yanayosemwa na wana UWT au kunamengine ambayo yamewapelekea anguko hili kubwa la aibu ndani ya chama huku ikieleza Cathereen Magige ni mzoefu na mekaa kwa zaidi ya miaka 18 bungeni au ndiyo kil mtu aonje keki ya Taifa au ndiyo kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi.






Comments