TLS KUENDELEA KUSAIDIA WANANCHI KUPITIA TAASISI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA.
Maswi ameyasema hayo leo Julai 23,2025 wakati akifungua Kongamano la msaada wa Kisheria kwa mwaka 2025, Kongamano linalofanyika Jijini Arusha likiwa na kengo la kuimarisha maswala mbalimbali ya utoaji wa haki kisheria.
"Kongamano hili ni jukwaa la kitaifa la mazungumzo, tathmini pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mfumo wa msaada wa kisheria nchini ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia". Amesema Maswi.
"Nia ya serikali ni kuboresha huduma ili kupata takwimu kamili juu ya kile tunachokifanya ya utoaji wa huduma ya kisheria kwa maana watanzania wanataka huduma bora kwa maendeleo ya taifa letu". Amesisitiza Maswi.

"Kongamano hili nisaidia kutekelezwa kwa utoaji wa mswaada wa kisheria kwa watu wote kwale watekelezaji waliyo vijijini na wale waliyo mijini itasaidia kutoa takwimu na kutoa taswira ya nini tusafanye na kuboresha ili kuongeza utoaji wa kisheria na sio kuwaachia watu wa maendeleo ya jamii na kuwasaidia wananchi". Hanifa.
Hanifa ameeleza kuwa mpaka sasa kumekuwa na matokeo makubwa ya wananchi kuamini serikali yao hasa katika maswala ya utoaji huduma ya msaada wa kisheria kwa kutatua changamoto zao mbalimbali.
"Kupata haki ya kisheria ni moja ya mahitaji ya msingi kwa mwanchi mwenye mahitaji maana ndiyo tumaini la upatikanaji wa haki maana itataluwa na mamlaka za utoaji haki na sisi kama TLS tutaendelea kushirikiana na Wizara ya Katiba ma Sheria kuhakikisha haki hii ya msingi inaendelea kupatika". Amesema Mwambukusi.
Mwambukusi ameeleza kuwa TLS inaendelea kupambania haki za wananchi wote hasa wapembezoni kupata msaada wa kisheria maana huko ndiko kuna mambo mengi ya mkanganyiko ikiwemo, ardhi,mirathi na saaa wameamua kushirikiana nawizara husika ili kuendelea kutoa haki.
Kongamano hilo la msaada wa Kisheria kwa mwaka 2025, linafanyika Jijini Arusha kwa siku mbili kuanzia leo leo Julai 23 hadi Julai 25, 2025, Kongamano ambalo limeudhuliwa na viongozi mbalimbali.
Comments
Post a Comment