ARUSHA ITAENDELEA KUWA NA AMANI SASA NA HATA BAADA YA UCHAGUZI. CPA. MAKALA.
Mkuu wa Mkoa huyo ameipongeza uongozi wa shule hiyo kwa kutambua na kuthamani kazi na jitihada zinazo fanya na serikali hasa katika kuwaletea maendeleo watanzania kitu ambacho ameeleza hakisemwi na watanzania wengi ila wao kama shule wameamua kuwafundisha vijana uzalendo kitu ambacho kitalinda taifa hili ha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2025.
"Nataka niwahakikishie kuwa mtasoma kwa amani, mtaishi kwa amani na uchaguzi utafanyika kwa amani". Amesema CPA. Makalla.
Katika swala zima la uchaguzi na juu ya ujumbe waliyokuwa wameubeba wanafunzi hao, CPA. Makalla ameeleza kuwa serikali kwasasa inafaya maboresho ya mitahala ili kuhakikisha ilimu ya Tanzania inakuwa yenye tija na kulenga katika kujiajili kitaifa na kimataifa ili kupunguza wimbi la ajira nchini.
Aidha Makalla ameeleza kuwa Tanzania ni nchi yenye amani duniani na kamwe amani hiyo haitakaa itoweke kwa sababu ya watu wachache wasio wazalendo na nchi hii na kuwahakikishia wanafunzi hao katika kipindi hiki cha uchaguzi amani itakuwa ya hali ya juu kwamba ameshajipanga yeye pamoja na kamati yake kuhakikisha wananchi wote wanapata nafasi ya kumchagua kiongozi wanao mtaka.
"Tunawahakikishia kwamba kuanzia sasa, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi nchi yetu itaendelea kuwa na amani na niwapongeze kwa kuadhimisha miaka 25 kwa kuhamasisha amani. Mkasome kwa amani na nchi yetu itaendelea kuwa na amani." Amesisitiza CPA. Makalla.
Awali katika maelezo ya wanafunzi hao wameeleza kuwa wameamua kufanya matembezi hayo ya amani wakitambua kuwa amani ndio msingi wa elimu, maendeleo na ustawi wa jamii.
Wameeleza kuwa bila amani elimu hukwama na mustakabali wao kama watoto watashindwa kufanikiwa, wakisema ni muhimu kila mmoja kufahamu kuwa kudumisha amani ni jukumu la kila mwananchi.
Aidha wanafunzi hao waliongozwa na Ujumbe wa Maadhimisho hayo ya miaka 25 ya Green Valley ukiwa ni kusisitiza kuhusu amani kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025.
Comments
Post a Comment