MANENO KUNTU KUTOKA KWA MBUNGE CHIKU ISSA KWA WATANZANIA.

🔻AFUNGUKA YA MOYONI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU HAPO KESHO OKTOBA 29.

Na Lucas Myovela.

Mbunge wa viti maalumu kwatiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) katika Mkoa wa Arusha Mhe. Chiku Issa amewaomba watanzania wote wenyesifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi kuweza kutimiza jukumu hilo la kikatiba la kuchagua viongizi mbalimbali.


Chiku ameyaeleza hayo leo Oktoba 28, 2025 katika andiko lake maalumu kwenda kwa watanzania kote nchini ambao ni wanachama wa chama cha mapindizi na wale ambao siyo wanachama wa chama hicho.


Chiku Athuman Issa aliteuliwa kuwa Mbunge wa viti maalum Mkoani Arusha mwishoni mwa mwezi wa nane (31 July 2025 ) kwa kuchaguliwa kwa kura 775 na kumpa ushindi nafasi ya pili nafasi ambayo inampeleka bungeni moja kwa moja.


ANDIKO LA AHSANTE YA CHIKU ATHUMAN ISSA.

Naanza kwa kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa Rehema na Fadhili zake zilizotuwezesha kuufikia Uchaguzi Mkuu katika siku chache zijazo.


Naungana na Watanzania wenzangu kumwomba Mungu atujaalie Uchaguzi Mkuu 2025 uliosheheni amani na utulivu kama zilivyokuwa chaguzi kuu zilizopita chini ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi, CCM, na watangulizi wake TANU na ASP.


Nachukua nafasi hii kuwasihi na kuwahimiza wananchi wote, wakiwemo wanaCCM, kujitokeza kwa wingi hiyo tarehe 29 Oktoba na kumpa kura za ‘Ndio’ Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Wabunge na madiwani wa CCM.


Kama ilivyokuwa zamani, na hata sasa, CCM imebaki kuwa chachu na nguzo kuu ya umoja, amani, upendo na maendeleo ya Watanzania wote.


Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza Amani na Usalama kama msingi wa maendeleo endelevu ya Taifa letu,Tuendelee kuipa imani CCM kwa kuipigia kura hadi kuichagua.


Ubunge wangu mteule ni matokeo na uthibitisho wa demokrasia iliyojaa ndani ya CCM. Kwa unyenyekevu mkuu na dhati ya moyo nasema ASANTE kwa Chama changu na jumuiya yake ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ngazi zote.


Ni CCM na UWT ndio walionilea na kunikuza mpaka nikateuliwa kupata dhamana hii ya Mbunge Mteule. Dhima ya nafasi niliyoteuliwa ni kulitumikia Taifa langu la Tanzania kwa kutekeleza Ilani ya CCM huku nikizingatia agenda ya maendeleo na maslahi ya wanawake, na hapohapo kuung’arisha na kuupaisha Mkoa wetu wa Arusha.


Kazi na Utu: Sote twendeni tukapige kura. Tumpe ‘Ndio’ Mgombea wa Urais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, na wabunge na madiwani wote wa CCM.


Ikumbukwe leo Oktoba 28, 2025 ndiyo mwisho wa kampeni kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini na hapo kesho Oktoba 29,2025 ndiyo siku ya kupiga kura ili kuweza kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Comments