TOYO WAPIGA TRAMPA WASHUSHIWA SHERIA KALI IKIWEMO FAINI YA MILIONI MOJA.

KERO YA GEREJI YA UMOJA YA MAFUNDI KROKONI YAPATA UFUMBUZI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Mkuu wa wila ya Arusha Ndg. Joseph Modest Mkude, Ametangaza vita na madereva wa pikipiki Jijini Arusha walinao toboa eksozi za pikipiki na kuwa na mliyo mkubwa maarufu kama (Trampa).

Mkude Ameyasema hayo leo Oktoba 22, 2025 wakati akiongea na mafundi wa Gereji ya Umoja wa mafundi Krokoni katika viunga vya Suye katika kata ya Kimandolu Jijini Arusha alipofika kusikiliza kero zao zinazo wakabili.


"Hii imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi na hii tabia inazidi kukua kila siku na hii inatokana na vijana wachache wasiyo na malezi bora kwa wazazi wao na badala ya kuchukua fulsa ya uendeshaji pikipiki kama ajira ila wao wanaona ni bora kukera watu". Amesema Mkude.


"Kwa sasa Arusha hii sheria ni moja tu tena kali akishikwa dereva toyo anayepiga kelele katikati ya mji faini ni shilingi Milioni moja ikiwezekana na kifungo, hii sheria itakuwa funzo kwa wengine tunataka mji utulie maana ni mji wa kitalii". Amesisitiza Mkude.

Aidha Mkude ameeleza kuwa katika changamoto zote walizoeleza kubwa ni changamoto ya miundonu hasa barabara ambayo ni korofi ambayo inaonekana kuwa hatarishi kwa shule ya sekondari pamoja na mazingira ya Gereji hiyo inayopeekekea kukwama kwa ufanisi wa kazi.


"Mmezungumza swala la mikopo, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshatoa fedha katika makundi yote kupata mikopo na hapa nitamuelekeza mtaalam aje mzungumze nae ili muweze kunufaika na mikopo hii ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na mitaji ya uhakika". Amsema Mkude.


Akitatua kero ambayo imekuwa sitofahamu kwa mafundi hao juu ya umiliki wa eneo hilo walilopewa ili kujenga Gereji toka mwaka 2006 ambapo kwasasa limeoneknaa kuw lulu kwa halmashauri ya jiji la Arusha na kulitaka kitu ambacho kinaonekana kuwa kero kwa mafundio mkude amewataka waunde umoja ili umiliki uwe katika umoja.


"Niwaombe mjenge jumuiya imara ili umiliki uende kwenye jumuiya na siyo mtu mmoja na halmashauri ibaki kama msimamizi napia natoa muda usio zidi mwezi mmoja wale wote waliyoletwa hapa na kuondoka wawe wamerejea maeneo waliyo pangwa tofauti". Amesisitiza Mkude.

Awali katibu wa Umoja huo ameeleza kuwa Mgogoro uliopo ni kuhusu vibanda walivyo jenga na kwasasa halmashauri kuvitamani na kutaka kutulipa elfu 15, kingine ni ubovu wa barabara ambapo mvua ikinyesha hakuna gari inayo pita kuingia gereji kitu kinachopelekea hata wanafunzi kupata tabu kuingia shule.


"Changamoto nyingine ni vijana kuwa wengi serikali iwafikilie vijana waliyo gereji japo kuleta mikopo na mashine ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi. Pia tunaomba serikali kutuamini na kutupa kazi ya kutengeneza magari ya serikali ili tuweze kupata kipato na kulijenga taifa moja". Amesema Katbu huyo


"Tangu kuanzishwa kwa gereji 2006 hakuna mikataba ya wazi na nyumba tulizo jenga mpaka sasa tunahofia kuchukuliwa na halmashauri, Tunaomba serikali kuangalia kwa jicho la pekee utoaji wa mitaji kwa mafundi wazee ili waweze kujikimu" Amesisitiza Katbu huyo.





Comments