🔻HAKUTAKUWA NA MAANDANO ZAIDI KWENDA KUPIGA KURA.
Mkude ameeleza hayo leo Oktoba 27, 2025 wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya namna walivyo jipanga kuhakikisha wakazi wa Jiji la Arusha wanapata nafasi ya kupiga kura kwa amani ma kuweza kumchagua kiongozi wanae mtaka katika uchaguzi mkuu unaotaraiwa kufanyika Mwezi Oktoba 29.2025.
Mkude ameeleza kuwa katika Jiji la Arusha wananchi wanaotarajiwa kupiga kura ni 435,119 ambapo tayari maadalizi ya vituo vya kupigia kura yananendelea na kutakuwa na vituo 1052 vya kupigia kura.
"Katika uchaguzi huu tumejipanga vizuri tunawahakikishia wananchi wa Jiji la Arusha watakuwa salama na watapiga kura kwa amani na watarejea makwao kwa amani pasipo vurugu yeyote". Amesema Mkude.
"Hatutegemei kuwa na maandamano maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alishazungumza hilo kwamba maandamano yawe ya kwenda kupiga kura na si vinginevyo". Ameongeza Mkude.
"Hakuta kuwa na uvunjifu wa amani, niwahakikishie wanachi wa arusha wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na wakimaliza watulie kusubilia matokeo maana sehemu ya kutangazia matoke zote zipo salama". Amesisitiza Mkude.
Aidha Dc Mkude ameeleza kuwa mpaka sasa hakuna chama chochote ambacho kimelalamika kufanyiwa vigusu vya aina yeyote na wamefanya kampeni zao kistarabu,kisheria na haki.
"Tuna mitaa 154 katika jiji letu la Arusha na vituo vya kupigia kura vipo vya kutosha ambapo mwananchi hata tembea umbali mrefu kwenda kupiga kura". Amesema Mkude.
"Vifaa vyote vya uchaguzi vimeshaingia na kila kitu kikosalama na miundombinu yote iko salana kwa makundi yote na usalama upo wa kutosha wa kulinda vifaa hivyo niwaombe wakazi wa Arusha wajitokeze Oktoba 29,2025 kwenda kupiga kura". Ameingeza Mkude.
"Sisi kazi yetu ni kulinda raia na mali zao, niwatoe wasiswasi wale wenye biashara zao kama watahitaji kufungua biashara zao baada ya kupiga kura wakafungue ulinzi upo wa kutosha". Amesisitiza Mkude.
Hata hivyo ikiwa imebaki siku moja ili kufika siku ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 mpaka sasa vyama vilivyosiriki katika kampeni hizo kwa jiji la Arusha ni vyama 16 kati ya vyama 17 vilivyochukua fomu huku chama kimoja kikiwa hakijarudisha fomu hadi sasa.


Comments
Post a Comment