WAFADHILI WAOMBWA KUJITOKEZA KUSAIDIA UENDESHAJI WA SHULE YA WASICHANA BETHSAIDA INAYOHUDUMIA WATOTO YATIMA.
🔻WAFADHILI TUPIENI JICHO LA UPENDO SHULE YA WASICHANA BETHSAIDA.Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Shule hiyo, Erasto Emmanuel, alisema shule hiyo inategemea zaidi misaada ya wafadhili, hasa kutoka nje ya nchi, lakini idadi yao imepungua kutokana na changamoto za dunia ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa Corona na vita kati ya Urusi na Ukraine.
Alifafanua kuwa kupungua kwa wafadhili kumesababisha udahili wa wanafunzi kushuka, kwani sasa analazimika kuchukua idadi ndogo ya watoto wanaoweza kuhudumiwa kwa rasilimali zilizopo.
Aidha, alitoa wito kwa wadau na wafadhili kujitokeza kufadhili watoto mmoja mmoja au kusaidia mahitaji muhimu kama chakula, vifaa vya kujifunzia na mishahara ya walimu ili shule iweze kujiendesha bila wasiwasi.
“Mwaka jana wanafunzi wote waliweza kuendelea na masomo, tulikuwa na idadi kubwa ya waliopata Division One na Two, huku waliopata Division Three wakiwa saba tu,” alisema Machary.
Aliongeza kuwa wanapanga kuendeleza miundombinu ya shule kwa kujenga majengo mapya kutokana na mahitaji makubwa, na kwamba upatikanaji wa wawekezaji utasaidia kufikia lengo hilo.
Aidha, alisema shule hiyo sasa inaelekeza nguvu zaidi katika mafunzo ya ufundi stadi ili kuwawezesha wanafunzi kujiendeleza na kujitegemea wanapomaliza masomo.
“Tunaiomba serikali na wafadhili watusaidie pia kupata fursa za kufanya ziara za kielimu katika maeneo mbalimbali ili kuongeza uelewa wetu,” alihitimisha Kivuyo.
Comments
Post a Comment