🔻AWATAKA WAPIGE KAZI KWA KUZINGATI MIHIMIKI YOTE MITATU NA KUACHA KUPIGANA SHOTI.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Aruaha CPA. Amos Makala amewataka madiwani wa Jiji la Arusha kutenda kazi kwa weledi kwa kuzingatia ahadi zao walizo zitoa kwa wananchi ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Makala ameyasema hayo leo Disemba 16, 2025 wakatika akizungumza na baraza la madiwani wa jiji la Arusha na kuwakumbusha kuwa serikali inawategemea kwa kiasi kikubwa ili kuhakikisha wananchi waweza kupata maendeleo ya alaka chini ya uongozi wa serikali ya Awamu ya sita.
Audha CPA. Makala amewataka madiwani hao kuwa na uchungu na uzalendo katika kusimamia miradi ya halmashauri hiyo ikamilike kwa wakati na yenye tija katika ukuaji na maendeleo ya jiji hilo kuwa ni mfano wa kuigwa.
"Katika kutimiza haya yote yanahitaji umoja na ushirikiano katika kuleta maendeleo hasa umoja nabushirikiqno baina yenu na wataalamu kwasasa uchaguzi umekwisha sasa ni kufanya kazi za wananchi maana ndiyo waajali wenu". Amesema CPA. Makala.
"Nyie mliyo madarakani yote ni mapenzi ya mungu ila mkishirikiana kwa pamoja mtapiga hatua katika maendeleo, Msiwekeane vinyongo wala kulipa visasi hiyo hatokuwa njia sahihi ya kuleta maendeleo kwa pamoja". Ameongeza CPA. Makala.
"Tunaanza kazi za kuwatumikia wananchi, tushirikiane, tuaminiane ma kikubwa zaidi msingi wa yote ni mapato muweke misingi ya kusimamia na uborehaji wa huduma katika maeneo mnano kusanya mapato ili muweze kufikia malengo yenu". Amesema CPA Makala.
Makala ameongeza kuwa kwasasa jiji la arusha linayo miradi mingi na mikubwa ambayo ni ya kiasasa na kimkakati kitu ambacho ni muhimu kwa maendeleo ya arusha.
Aidha katika sekta ya michezo CPA. Makala ameosema kuwa kasasa arusha inahitaji kuwa ma timu ya mpira inayo milikiwa na jiji la Arusha kutokana na ujenzi wa viwanja vya mpira vya kisasa vinavyo jengwa ndani ya jiji hilo.
"Nendeni mkawashuru wananchi sasa na kufanya nao kazi maana wewe ndiyo mbeba maono yao na ndiyo kazi uliyo iomba kwao ili kuwatatulia changamoto zao msibaki nyuma kwa kusubikia mpaka mpate pesa ndiyo mwende mtakutana na mambo mengi, twendeni sasa tukawatumikie wananchi wetu". Amesema CPA . Makala.
"Katika maendeleo yote lazima tuangalie barabara zetu za ndani pasipo miundombinu thabiti hatutaweza kufikia malengo tunayo yahitaji na kwenye hili niwaagize tarura kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiqna na diwani wa kata husika ili kupunguza changamoto ya miundombinu ya barabara zetu za ndani". Ameongeza CPA. Makala.
Kwa upande Meya wa jiji la Arusha Maximilian Iranqe amesema kuwa wanavyanzo viinne vya mapato hasa katika sekta ya utalii ambapo ni utalii wa uhifadi, michezo, mikutano na utalii wa kimatibabu.
"Kwa kupitia kituo chetu cha Afya cha kaloleni tumeshapokea zaidi ya wageni 100 kutoka mataifa mengine na kwasasa tunaujenzi wa OPD ambao jengo hilo linaweza kutua helkopta ili kuwapa wqgeni unafuu wanapo patwa na matatizo ya kiafya kutoka katika hifadhi zetu". Amesmema Iranqe
"Kupitia mipango na mikakati tumejipanga Arusha kuendelea kuwa safi na tumekubaliana madiwani wote kila jumamosi madiwani kwa kushirikiana na wananchi kufanya usafi pia tunaitazama Arusha katika sekta ya viwanda". Ameongeza Iranqe.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude amesema Katika kila hatua wanategemea Jiji la Arusha kujengwa kwa kupitia nguzo tatu zote ambao ni madiwani, wataalamu na serikali kuu kwasasa tunaimani madiwani hawa wakiungana kila mmoja kusimamia majukumu na mipaka yake ya kiutendaji.
"Kwasasa hatutegemei malumbano katika halmashauri hii kutokana na mikakati mliyo jiwekea kwa kutambua hilo naamini kwa maeleno na mashirikiano ni imani yangu mtachapa kazi na Jiji letu likaendelee kung'ara". Amesema Mkude.






Comments
Post a Comment