TRA YAMSHUKURU MKUU WA MKOA WA ARUSHA KWA USHIRIKIANO MZURI.
Ziara hiyo imefanyika kama sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano kati ya TRA na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato Mkoani hapo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Makalla akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndugu Misaile Mussa wameipongeza TRA kwa kuendelea kutoa Elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, huku wakisisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa jukwaa maalum la wadau kutoka sekta mbalimbali ili kukuza uelewa wa pamoja ili kuongeza mapato ya Serikali.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha, Bw. Deogratius Shuma, ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili walipakodi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali, hatua itakayosaidia kujenga taswira chanya ya taasisi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Aidha, Mhe. Makalla ameishukuru TRA kwa kuendelea kuboresha mifumo na huduma za kielektroniki, akibainisha kuwa maboresho hayo yamerahisisha ulipaji kodi kwa wakati na kuongeza ufanisi katika utoaji wa Huduma.









Comments
Post a Comment