WANANCHI WALIYOPISHA ENEO UJENZI WA UWANJA WA MPIRA AFCON ARUSHA WALAMBA BILIONI 2.3.

🔻SERIKALI KUENDELEZA TASNIA YA MICHEZO KIMATAIFA ZAIDI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Leo Disemba 31, 2025 imekabidhiwa hundi ya Mfano yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3 kwa wakazi wa kata ya Matevesi Jiji Arusha waliyo weza kutia maeneo yao ili kuweza kupisha ujenzi wa uwanja wa Mpira maalufu uwanja wa AFCON.


Akikabidhi hundi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA. Amos Makala, amesema ni fahari kubwa kwa watanzania kuwa wazelendo katika swala zima la maendeleo na ujenzi wa taifa kitu kinacho chochea ukuaji wa uchumi kama ilivyo fanywa na wananchi hao waliyo iacha ardhi yao kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu utakaotumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.


CPA, Makala alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa sambamba na kulinda maslahi ya wananchi pasipo kuacha kutoa fidia endapo miradi hiyo itagusa maeneo ambayo tayari yanamilikiwa na wananchi.


"Malipo ya fidia ni haki ya msingi na yanapaswa kulipwa kwa wakati, kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria kama leo hii tunavyo fanya hapa ili waliyoweza kuachia maeneo yao waweze kwenda kununua sehemu nyingine na kufanya maendeleo yao ya kijamii". Ameeleza CPA, Makala.


“Maendeleo hayawezi kusimama, lakini hayawezi pia kuwanyanyasa wananchi, ndiyo maana leo tunakabidhi fidia hii kwa wananchi waliopisha ujenzi wa uwanja wa AFCON 2027,” Aliongeza CPA,Makala.


Aidha Mkuu wa Mkoa huyo aliweza kupata nafasi ya kukagua ujenzi wa uwanja huo kwa hatua uliyofikia katika ujenzi na kuendelea kuwapongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa usimamizi wa karibu kwa kushirikiana na shirikisho la mpira hapa nchini pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Ndg, Joseph Mkude, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuiamini Mkoa wa Arusha katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa AFCON 2027, ambao utafungua fursa za kiuchumi, ajira na maendeleo ya michezo kwa vijana wa Arusha na Taifa kwa ujumla.


Pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa ziara yake ya kikazi wilayani Arusha, iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa AFCON 2027 pamoja na kushuhudia na kuzindua zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huc mkubwa wa kimkakati.


Aidha Mkude Vkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa Wilaya ya Arusha itaendelea kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na taasisi zote husika ili kuhakikisha maandalizi ya AFCON 2027 yanafanyika kwa viwango vinavyokubalika kimataifa, ikiwemo kukamilika kwa huduma muhimu kama maji na umeme kwa wakati.


Hafla hiyo imefanyika katika eneo unapojengwa uwanja huo na kudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi.


Tukio hilo ni ishara ya dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha haki za wananchi zinalindwa wakati wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ya taifa.








Comments