WAZIRI MAVUNDE ATOA SIKU 7 KWA KATIBU MKUU KUKAMILISHA VIBALI VYOTE VYA MRADI WA JENGO LA KUONGEZA THAMANI MADINI JIJI ARUSHA NA UTOAJI WA BOMBA LA MAJI ILI KUPISHA MRADI, AMTAKA MKANDARASI KUFANYA KAZI MASAA 24.
đź”»UJENZI WA JENGO LA KITUO CHA MAFUNZO YA KUONGEZA THAMANI MADINI YA VITO WAANZA JIJINI ARUSHA.
■Mradi huu ni mkakati wa kuhakikisha madini vito yanaongezewa thamani nchini, Ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais. Dkt. Samia katika kuendeleza mnyororo wa madini thamani hapa nchini ma kuhakikisha vijana wa kitanzania wananufaika.
Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza mikakati yake kwenye mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini ya vito kama Sera ya Madini ya Mwaka 2009 inavyoelekeza.
Sambamba na hapo, Waziri Mavunde amesisitiza kuwa, kuanza kwa ujenzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia Bunge la 13 jijini Dodoma.
Waziri Mavunde amebainisha kuwa, kukamilika kwa kituo hicho , kutaleta faida mbalimbali ikiwa pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi watakao jiunga kwenye kituo, kuongezeka kwa wataalamu wa uongezaji thamani madini ya vito, kufungua fursa za ajira kwa vijana na wafanyabiashara wa madini , pamoja na kutosafirishwa kwa madini ghafi nje ya nchi hivyo kutachagiza ongezeko la mapato kwa taifa.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Mavunde ametoa siku 7 kwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini kukutana na wakandarasi ,TGC na Taasisi za serikali kwa ajili ya upatikanaji vibali muhimu vya kuendeleza ujenzi.
Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya Arusha Mhe. Joseph Mkude ameahidi kuendelea kufuatilia maendeleo ya ujenzi ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kama Serikali inavyotaka.
Mkude ameongeza kuwa, kukamilka kwa kituo hicho itakuwa moja ya sehemu ya uwekezaji mkubwa wa serikali husasan kwenye Sekta ya Madini mkoani Arusha.
Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi, Mkuu wa kituo cha TGC Mhandisi. Ally Maganga ameeleza kuwa, ujenzi wa majengo pacha hayo ya ghorofa 8 utagharimu Tsh Bilioni 33 na kukamilika kwake kutaongeza fursa ya vijana wengi kupata ajira kupitia ujuzi wa uongezaji thamani madini ya vito.
"Kwasasa kilicho tukwamisha kwa kiasi kikubwa ni vibali hasa utoaji wa bomba kubwa la maji kutoka mamlaka ya maji safi Jiji la Arusha (AUWSA) kitu ambacho kinatunyima eneo la ufanisi wa kazi, lakini badala ya kukaa tumeamua kuanza kazi upande ambao upo wazi nasasa tumeshusha nondo tani 200 kwaajili ya kuanza kazi hii mara moja". Amesema Eng. Lubuva.
Kukamilika kwa mradi huu unachagizwa kuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika sekta ya madini hasa katika uongezaji wa thamani ya madini ya vito hapa nchini na utoaji wa fursa kwa vijana hapa nchini.

.jpg)








Comments
Post a Comment