🔺️ATAKA UADILIFU WA FEDHA KWA VIONGOZI, AZANIA BENKI YACHOCHEA UCHUMI SEKTA YA MIKOPO.
Katika kuunga mkono juhudi za madereva kupata leseni, Mkude alipendekeza mpango ambapo waendesha bodaboda wachangie nusu ya gharama ya leseni huku yeye akiahidi kushirikiana na wadau kulipia nusu iliyobaki. Madereva wametakiwa kujiandikisha kwa majina ili kurahisisha utekelezaji wa mpango huo.
Mkude pia alisisitiza kuwa operesheni ya kudhibiti pikipiki zinazokiuka sheria itaendelea, hasa kwa wale wanaosababisha vurugu mitaani kwa kuendesha hovyo au kupiga mafataki.
Aidha, Mkuu wa Wilaya aliagiza Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kuondoa urasimu na ukiritimba katika utoaji wa leseni kwa waendesha bodaboda.
Amesema tayari operesheni zimefanyika katika maeneo mbalimbali, ambapo waendesha bodaboda waliokiuka sheria wakiwemo wasio na leseni na wasiovaa helmeti, wamekamatwa na hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.
Jeshi la Polisi limewataka waendesha bodaboda kushirikiana na mamlaka na viongozi wao, likisisitiza kuwa bodaboda ni ajira halali na muhimu, lakini lazima iendeshwe kwa kufuata sheria, kuheshimu jamii na kulinda usalama kwa wananchi ambao ndiyo wateja wao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Bodaboda Jiji la Arusha, Shwahibu Hamisi, alisema umoja wao umeingia makubaliano na kampuni ya TVS kwa ajili ya kuwakopesha wanachama pikipiki. Kwa awamu ya kwanza, pikipiki 20 tayari zimekopeshwa bodaboda
Aidha, Hamisi alimwomba DC Mkude kusaidia Wilaya ya Arusha kurejeshewa zaidi ya shilingi milioni 68 zinazodaiwa na Umoja wa Bodaboda wa Mkoa wa Arusha, fedha ambazo zinakusudiwa kutumika kununua pikipiki zaidi kwa ajili ya wanachama.
Mradi wa kukopeshana pikipiki unatajwa kuwa hatua muhimu katika kuwawezesha kiuchumi waendesha bodaboda na kuboresha usalama barabarani katika Jiji la Arusha.









Comments
Post a Comment