DKT. KIJAJI AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI TAWA, AWAPA MAJUKUMU YA KUPANDISHA MAPATO ILI KUIMARISHA UHIFADHI.
🔺️AWAPONGEZA KWA UTENDAJI BORA, AITAKA BODI KULETA MWANGAZA WA KISERA KATIKA SEKTA YA UTALII NA UHIFADHI.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameitaka bodi mpya ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA kuongeza mapato ili kuimarisha uhifadhi na kuvutia watalii zaidi, huku serikali ikilenga kufikia watalii milioni nane ndani ya miaka mitano ijayo ilikufikia dira ya Taifa 2050."TAWA ni miongoni mwa Taasisi zetu zilizo chini ya Wiazara ya Maliasili na Utalii yenye majukumu makubwa ambapo toka kuqnzishwa kwake hadi leo hii imeleta mabadiliko na mageuzi makubwa katika sekta uhifadhi na utalii na inaendelea kufanya vizuri zaidi". Amesema Dkt. Kijaji.
"Mapato yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 75.6 hadi bilioni 87.32 mwaka wa fedha 2024/2025, lakini bado hayajaakisi kikamilifu jukumu la TAWA, Niitake bodi itafute vyanzo vipya vya mapato na kuanza kutoa gawio kwa serikali kuanzia mwaka huu wa fedha 2026/2027". Amesema Dkt. Kijaji.
Aidha Dkt. Kijaji ameikumbusha bodi hiyo kuzingatia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya Dira ya Taifa ya 2050 inayotazama sekta ya utalii kama chanzo kikuu cha ajira kwa vijana wa Kitanzania.
"Nina iagiza Bodi kuhakikisha TAWA inatekeleza majukumu yake kwakuzingatia shabaha na malengo ya dira hiyo, kwa ujumla dira imetambua kuwa utalii ni miongoni mwa sekta zenye uwezo mkubwa katika kukuza ajira, kuongeza mauzo ya nje na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine". Amesisitiza Dkt. Kijaji.
Pia ameisisitiza TAWA kuendelea kuangalia namna kudhibiti wa wanyama wakali na kwa kutoa ushirikiano katika sekta binafsi hasa katika miundombinu ya barabara ambazo zipo pembezoni mwa hifadhi na hifadhini ili wanyama hao wasiwe kikwazo.
"Kila mwaka bodi ilete taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na Dira ya Taifa ya 2050, ni imani yangu mnao uzoefu wa kutosha maana kwasasa TAWA ina miaka 10 tangu kuanzishwa kwake". Amesema Dkt. Kijaji.
"Serikali inatarajia bodi hii kuleta mwelekeo unaoakisi sera, siasa na mahitaji ya sekta ya utalii na uhifadhi, ili kuongeza tija na mchango wa TAWA kwenye uchumi wa taifa.” Amesema Nkoba.
"Nitahakikisha baadi ya maeneo yetu ni maeneo ambayo vijana wanakwenda kuto stress wanakwenda kufurahia na tumeanza hivyo lakini kwenye mpango yetu tutaweka vitu mbalimbali ikiwemo sehemo za watoto kufurahia ili tuhakikishe kwamba wananchi wanafurahia uhifadhi wa taifa lao ikiwemo kuimarisha sehem mbalimbali za utalii kuhakikisha wananchi wa kipato chote wanatembelea". Amesema Semfuko.
Aidha Semfuko ameeleza kuwa wao kama TAWA wamejiwekea mikakati ya miaka mitatu kuhakikisha uhifadhi unaimarika na mapato yanaongezeka na TAWA inachangia kikamilifu maendeleo ya taifa kwa kutoa gawio nono kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kuzinduliwa Bodi mpya ya nne ya TAWA inachagiwa sasa kuanza kazi huku macho ya serikali na Watanzania yakielekezwa kuona kama TAWA itaibuka kuwa mhimili wa mapato, uhifadhi na ajira katika safari ya kuelekea uchumi wa utalii na kuzingatia Dira ya Taifa 2050.












Comments
Post a Comment