MEYA JIJI LA ARUSHA ATOA MASAA 3 KWA KAIMU MKURUNGENZI KUONDOA TAKA SOKO LA MBAUDA, AGIZO LATEKELEZWA NDANI YA DAKIKA 15 NA SEKUNDE 25.
🔻ADAI HAKUNA MUDA WA KUBEMBELEZANA TENA ATAKA KILA KIONGOZI WA JIJI AFANYE KAZI ZA KUWAHUDUMIA WANANCHI.
Iranqe alionekana kukwerwa na harufu kali na mrundikano wa taka nyingi ngumu zilizo kwenye kontena la uchafu kitu ambacho wafanya biashara hao walieleza kuwa taka hizo hukaa kwa muda wa wiki mbili au zaidi na kunyeshewa na mvua kitu ambacho ni hatali kwa afya zao kutokana na magonjwa ya mlipuko.
"Natoa maelekezo kwako kaimu mkurugenzi wa Jiji la Arusha kutoa kontena la uchafu katika soko la Mtumba Mbauda kwa masaa 3 tu narudi hapa nisilikute". Amesema Iranqe.
"Huu sio wakati wa kubembeleza tena sasa ni wakati wa kufanya kazi nataka Jiji la Arusha iwe nafasi ya kwanza kila mwaka huu sio wakati wa kufanya siasa tena". Amesisitiza Iranqe.
Aidha katika katika hatua nyingine Mstahiki Meya wa jiji la Arusha ameeleza kuwa kwasasa katika karne ya 21 mataifa mengine yapo kwenye teknolojia Tanzania bado tupo kwenye kuhamasishana usafi wa mazingira na kuuliza kuwa je huko kwenye teknolojia tutafika lini.
Pia Iranqe, ameagizwa kuitwa kwa kikao cha maafisa tarafa na mawakala wa kuzoa uchafu ili aweze kujua ni kwanini wanakuwa wazembe katika usimamizi wa usafi na mazingira ndani ya jiji la Arusha.
Pia amemuelekeza katibu wa soko kuwa ni marufuku kufanya biasha katika masoko pasipo kufanya usafi na baada ya kumaliza biashara lazima wafanye usafi.
Aidha Iranqe ameagiza kutozwa faini za wale wanao kaidi waendelee kupigwa faini na kama wakiendelea kukaidi waondolewe sokoni ili kupisha wanao weza kufanya kazi na biashara kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizo wekwa.
"Soko hili nimeambiwa pia wanalipa ushuru nikutake Mkurugenzi na madiwani kurudi kukaa kuqngalia namna ya ushuru wao wanao lipa liwezwe kulekebisha soko hili au kujenga soko jipya na la kisasa". amesema Iranqe.
Kwa upande wake Diwani Kitomary Godgrey wa kata ya Sombetini Jijini Arusha ameeleza kuwa Changamoto kubwa inayowasumbua ni kontena linalotumika kukusanyia uchafu na kisha kupelekwa dampo limekuwa na uchafu mwingi na tukochukuliwa hadi uchafu kutoa harafu chafu soko zima la nguo Mbauda.
Pia amewataka wafanyabiashara wa soko hilo na wananchi kwa ujumla wa kata hiyo kuhakikisha wanafanya usafi ili kuweka mazingira safi na kundeleza juhudi za serikali katika sera ya mazingira.
Nae Diwani wa Daraja Mbili Mhe. Collins, ameeleza kuwa Wananchi ndiyo kiini cha yote yale na wao kama viongozi kazi yao ni kusimamia sheria walizo weka wenyewe ili kuendana na sera za mazingira nakuwataka wafanyabiashara kujiwekea tabia jema ya usafi ni rahisi mazingira.







Comments
Post a Comment