MEYA WA JIJI LA ARUSHA ACHAFUKWA ATOA MAAGIZO MAKALI KWA WATAKAO TUPA TAKA HOVYO MTAANI WASHUGULIKIWE KISAWASAWA.

🔻WATENDAJI KATA NA MAAFISA AFYA KUKIONA CHA MOTO ADAI SASA NI MUDA WA KUCHAPA KAZI.

Na Lucas Myovela - Arusha. 

Leo Januari 2, 2026 Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximikian Iranqe amezindua rasmi kampeni ya Usafi wa kata kwa kata zote za jiji hilo kwa lengo la kuweka Jiji hilo safi katika maeneo yote na kuendelea kuwa kivutio kwa watalii na kutoa maagizo makali kwa watakao kamatwa wanatupa taka hovyo ndani ya jiji hilo.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo uliyo ambana na ufanyaji wa Usafi katika soko dogo la Dampo katika kata ya Sokoni one, Iranqe amesema kuwa kwasa wanajipanga kuweka sheria ndogo za mazingira ili kuweza kudhibiti utupaji wa taka hovyo kitu kinacho sababisha jiji hilo kuwa chafu na kutoa maagizo kwa watendaji wa kata na mitaa pamoja na maafisa Afya kuhakikisha wanasimamia maeneo yao ipasavyo.


"Mwaka 2020 kipindi naanza udiwani nilivyokuwa meya nilikuta Jiji letu la Arusha ni la mwisho katika swala la usafi kwenye majiji yote hapa nchini lakini hadi mwaka 2025 tumekuwa wa kwanza na kuoata tuzo mbalimbali, Leo 2026 tumezindua rasmi zoezi hili la usafi katika jiji letu na kila eneo linalo fanyiwa biasha hakikisheni lina kuwa safi". Amesema Iranqe.


"Nakuagiza afisa Mazingira wa Jiji na maafisa Afya wa kata na mitaa, Watendaji wa Kata na mitaa kusimamia maeneo yao ipasavyo na kuhakikisha wananchi wote kufanya usafi katika maeneo yao na nyumba zao kutunza uchafu wanao uzalisha katika nyumba zao". Amesema Iranqe.


Pia amemuelekeza afisa mazingira wa jiji la Arusha kuhakikisha anasimamia vyema kandarasi ya wazoaji taka kuhakikisha magari wanayo tumia yanakuwa sio chanzo cha usambazi wa uchafu barabarani kama ambavyo hivi sasa inalalamikiwa na wengi.


"Afisa mazingira nakuelwkeza tena kukaa na mtu aliyeshinda tenda ya uchafu kuhakikisha gari zinazo zoa toka zinatumika kulichafua jiji maana likitembea linadondosha taka barabarani maana kama hana magari ya kisasa angalieni namna ya kuvunja mkata nae ili kupata mtu mwenye sifa". Amesema Iranqe.


"Naelekeza kwa kila mwananchi wa jiji hili la arusha awe mlinzi wa mwenzie kila anaye tupa taka hovyo aadhibiwe haswa ili kuendelea kulinda Jiji letu kuwa safi maana pasipo kuwashika adabu hawa wanao tupa taka hovyo wataendelea kuchafua miundombinu tunayo ijenga na mazingira yote kwa ujumla". Amesema Iranqe.


Aidha katika maendeleo ya miundombinu ya mitaro na barabara za ndani Iranqe ameeleza kuwa mpaka sasa halmashauri ya Jiji la Arusha wamejipanga kuandaa miundombinu ya mitaro na mifereji yote inayohitajika katika maeneo yanayo tuzunguka ili kuondokana na changamoto za mafuriko katika kipindi cha mvua za msimu wa mwezi wa tatu.

Kwa upande wake diwani wa kata ya sinoni Peter Inyasi, amesema kwamba katika usafi wa kata zilizo pembezoni mwa jiji ni hafifu kutokana na ujenzi holela wa nyumba za makazi kwa kutozingatia plani ya mipango miji kitu ambacho kinafanya magari ya kuzoa taka.












Comments