TARURA YAFUTA STEDI BUBU ZOTE ARUSHA ZINAZO SABABISHA FOLENI KATIKATI YA JIJI, WALIZIJENGA KAMA VIOTA SASA NI KILIO.

🔺️RC MAKALLA AIAGIZA TARURA, TANROAD NA POLISI KUONDOA FOLENI JIJI LA ARUSHA.

Na Lucas Myovela - Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameiagiza Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Arusha, Jeshi la Polisi pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushughulikia kadhia ya foleni kwenye Jiji la Arusha kwa wakati ili kuondoa vikwazo katika shughuli za kila siku za kiuchumi na Kijamii ndani ya Jiji la Arusha.

Katika kutekeleza agizo hilo, leo Jumatano Januari 14, 2026, kimefanyika kikao kilichowahusisha Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, TARURA, LATRA, TANROAD, Polisi na Idara ya Mipango Miji Jiji la Arusha, ambapo pamoja na mambo mengine wametangaza kufutwa kwa Vituo vya Mabasi katikati ya Jiji ambavyo vimekuwa vikitumika kushusha na kupakia abiria, wamiliki wa mabasi wakiagizwa kutumia Kituo Kikuu cha mabasi Arusha kwaajili ya abiria wao.


Kulingana na Mhandisi Julius Kaaya, Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha akizungumza kwaniaba ya washiriki wa Kikao hicho, agizo hilo linaanza utekelezaji wake mara moja, wakitangaza kuchukua hatua kali za kisheria kwa kampuni ya mabasi itakayokaidi kutekeleza agizo hilo.

Amefafanua kuwa baadhi ya Kampuni za mabasi yaendayo mikoani yameweka ofisi kwenye makazi ya watu ambad hupakia na kushusha abiria jambo ambalo limekuwa likisababisha kero kwa wananchi ikiwepo msongamano wa magari.


Kutokana na changamoto ya msongamano wa magari Jijini Arusha unaosababisha foleni, tumepokea maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kudhibiti changamoto hiyo utekelezaji wa agizo hilo, ambao unaanza mara moja na kubainisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa Kampuni itakayokaidi agizo hilo.


"Kulingana na Sheria Kampuni zote za mabasi haziruhusiwi kutumia majengo ya najazi ya watu na biashara jama vituo vya mabasi, kila basi linatakiwa kuanzia na kumalizia safari zake kwenye kituo kikuu cha mabasi Arusha".


Kwa upande wake Afisa Mipango Miji Jiji la Arusha Bi. Doroth Absalom ameeleza kuwa kulingana na sheria, Kampuni za mabasi haziruhusiwi kutumia majengo ya makazi na biashara kama Vituo vyao vya mabasi, akisema ni sheria kwamba kila Basi kuanzia safari zake kwenye Kituo Kikuu cha mabasi Arusha, akionya pia kuhusu uoshaji holela wa mabasi pembezoni mwa barabara.



Comments