WANANCHI ZAIDI YA 500 WALIPWA FIDIA YA BILIONI 3.2 KUPISHA UJENZI WA BARABARA YA MIANZINI - NGARAMTONI.
🚨WANANCHI ZAIDI YA 500 WALIPWA FIDIA YA BILIONI 3.2 ILIKUPISHA UJENZI BARABARA YA MIANZINI - NGARAMTONI KUKAMILIKA KWAKE KUNAWEKA HISTORIA MPYA ARUMERU.
🔺️TANROADS YAPEWA KONGELE KWA USIMAMIZI MAKINI WA UJENZI HUO SASA WANANCHI KUTEMBEA KIFUA MBELE.
"Arusha ni mji wa utalii unaopokea wageni wengi hivyo Serikali waelimisheni wananchi ili wafahamu kuwa barabara, madaraja na taa ni za wananchi hivyo wazitunze na kuondoa dhana kuwa miradi ya maendeleo ni ya Serikali", amesema Eng. Kasekenya.
Pia amemtaka Mkandarasi kutoka kampuni ya STECOL COOPERATION anaejenga mradi huo kuhakikisha unakamilika ifikapo Julai mwaka huu kama Mkataba unavyosema,jambo ambalo mkandarasi aliahidi mradi huo kukamilika kwa wakati ila akasisitiza kulipwa fedha zilizobaki ,naibu waziri aliwataka hazina kuhakikisha fedha za mkandarasi huyo zinalipwa kwani serikali ilishakamilisha malipo yote.
"Zaidi ya shilingi bilioni 23 zinatumika kujenga barabara hii ili kulifungua jiji la Arusha, kupunguza msongamano na kulipendezesha ili kuwa jiji la mfano na kuvutia wageni na matukio mbalimbali nchini", amesisitiza Naibu Waziri huyo wa Ujenzi.
Katika hatua nyingine Eng. Kasekenya amekagua ujenzi wa daraja la Tanganyeti lenye urefu wa mita 40 katika barabara kuu ya Arusha -Namanga na kuelezea kuridhishwa na kasi ya mradi huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 95.
Masawe alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng Godfrey Kasekenya, aliyefika kukagua maendeleo ya mradi mzima wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa-Sambasha hadi Ngaramtoni Km 18 inayojengwa kwa gharama ya sh,bilioni 23.
Akizungumza jana katika ziara hiyo, Masawe alieleza kuwa awali kipande hicho cha barabara hakikuwahi kujengwa kabisa, jambo lililoilazimu TANROADS kulipa fidia ili kupata eneo la ujenzi ndani ya hifadhi ya barabara.
“Mheshimiwa Naibu Waziri, fidia yote imelipwa kikamilifu na mkandarasi tayari yupo kazini. Baada ya hatua hii, TANROADS itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika,” alisema Masawe.
Alifafanua kuwa hadi sasa, ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita tatu umekamilika, kuanzia barabara ya Arusha–Manga hadi eneo walilofikia sasa.
Sambamba na hilo, mitaro ya maji imejengwa pande zote mbili za barabara kwa kuzingatia jiografia ya eneo hilo lenye milima na mvua nyingi wakati wa masika.
Kwa upande wa miundombinu ya maji, alisema kuwa makalvati makubwa saba yalipangwa kujengwa na yote tayari yamekamilika.
Aidha, kati ya makalvati madogo 39 ya mabomba, 36 yamekamilika huku ujenzi wa matatu yaliyobaki ukiendelea.
Katika utekelezaji wa mradi huo, Meneja huyo wa TANROADS alisema sera ya Wizara ya Ujenzi ya kuajiri wananchi wa maeneo yanayozunguka mradi imezingatiwa, ambapo hadi sasa zaidi ya wananchi 200 wamepata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, hatua iliyosaidia kuongeza kipato cha familia zao.
Akizungumzia gharama za mradi , Masawe alisema mkataba wa ujenzi una thamani ya shilingi bilioni 23, na kwamba kwa sasa mkandarasi hana madai yoyote ya fedha kwa Serikali.
“Serikali imelipa malipo yote kwa mujibu wa kazi zilizotekelezwa, na malipo yanaendelea kufanyika kulingana na uthibitisho wa kazi (certificates) kama inavyoelekezwa kwenye mkataba,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa mradi huo unasimamiwa na TANROADS kupitia Kitengo cha Baluchi Chakeku, ambacho ndicho msimamizi mkuu wa ujenzi.
Masawe alisema endapo hakutajitokeza changamoto kubwa, mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, kama ilivyobainishwa kwenye mkataba wa ujenzi.











Comments
Post a Comment